Publia wa Antiokia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Publia wa Antiokia alikuwa mwanamke Mkristo wa karne ya 4 wa huko Antiokia, leo nchini Uturuki, ambaye, baada ya kuishi katika ndoa na kuzaa mtoto mmoja, aliofiwa mumewe alijiunga na monasteri akawa abesi wake.

Ni maarufu kwa kuongoza masista wenzake kumpinga kaisari Juliani Mwasi hadi akapigwa na kudhalilishwa naye[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Oktoba[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.