Programu ya matumizi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Programu ya matumizi (pia: Apps za simu za mkononi) ni programu za kompyuta zinazotumiwa hasa na simujanja na saajanja na ni tofauti na zile zinazotumiwa na kompyuta.

Mwaka 2009 mwandishi wa makala za teknolojia David Pogue alisema kuwa simujanja mpya zitapewa jina la utani "app phones" ili kuzitofautisha na simu zilizotangulia.[1].

Neno "app", ambalo ni kifupi cha "software application", limekuwa maarufu toka wakati huo. Mwaka 2010 neno hili liliteuliwa na American Dialect Society kuwa "Neno la Mwaka".[2]

Programu hizi zina manufaa makubwa kwa watumiaji wa simujanja kwa masuala kama ya muziki, video, michezo kama vile pokeman[3], vitabu, habari, afya, biashara, n.k. Hata hivyo, apps hutumika visivyo pia kwa masuala kama vile wizi wa taarifa za siri, wizi wa nenosiri, matumizi ya mtandao wa intaneti bila ruhusa au malipo.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Pogue, David. "A Place to Put Your Apps", New York Times, November 4, 2009. Retrieved on January 22, 2013. 
  2. "App" voted 2010 word of the year by the American Dialect Society (UPDATED) American Dialect Society. Americandialect.org (2011-01-08). Iliwekwa mnamo 2012-01-28.
  3. Jackson, Anthony A. (2018-11-01), "Pokemon Jupiter Rom – The Full Story", Original Console Games (in en-US), retrieved 2018-11-29 
  4. Wifi Hacker app