Paulo Liu Jinde

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wafiadini Wakatoliki wa China.

Paulo Liu Jinde (Lanziqiao, 1821 hivi - Lanziqiao, 13 Julai 1900) alikuwa mlei wa China aliyefia Ukristo wakati wa Uasi wa Waboksa.

Akiwa mzee, dhuluma yao ilikuwa imemuacha yeye tu kati ya Wakristo wa kijiji chake. Hapo aliwaendea watesi hao akishika mikononi rozari na kitabu cha sala, akawasalimu Kikristo na kwa sababu hiyo aliuawa nao mara moja [1].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, ila ya kwake mwenyewe tarehe 13 Julai[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.