Nenda kwa yaliyomo

Paulo I wa Konstantinopoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ndogo kutoka Menologion ya Basili II.

Paulo I wa Konstantinopoli (mzaliwa wa Thesalonike, Ugiriki, alifariki mwaka 350 hivi), alikuwa askofu wa sita wa Konstantinopoli kuanzia mwaka 337.

Paulo alijihusisha na mabishano kuhusu Uario yaliyoshughulikiwa na ndugu Makaisari Constans I (Dola la Roma Magharibi) na Constantius II (Dola la Roma Mashariki).

Basi Paulo alitawazwa na kuondolewa mara tatu kati ya miaka 337 na 351.

Hatimaye aliuawa akiwa uhamishoni huko Cucusus, mkoani Kapadokia (leo nchini Uturuki).

Anaheshimiwa tangu kale kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Juni au tarehe 6 Novemba[1].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.