Paul Slabolepszy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Paul Slabolepszy
Amezaliwa 1948
Bolton, Uingereza,
Kazi yake Mwigizaji



Paul Slabolepszy (au Paul "Slab"; alizaliwa Bolton, Uingereza, 1948) ni mwigizaji na mwandishi wa tamthilia nchini Afrika ya Kusini.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Slabolepszy alizaliwa na mama Mwingereza na baba mkimbizi kutoka Polandi. Familia hiyo baadaye iliruhusiwa kuhamia Afrika ya Kusini.

Alilelewa na kukulia katika miji ya Musina, Pietersburg na Witbank. Slabolepszy alikwenda kusoma shule ya bweni ya Kanisa Katoliki, College of the Little Flower huko Polokwane.

Ndoto yake ya awali ilikuwa kuja kuwa mtangazaji wa michezo redioni. Wakati shuleni wakicheza mpira wa miguu, alikuwa mchambuzi wa mchezo na alikuwa akirekodi kw aajili ya kusikiliza tena baadaye. Maoni yake yakaja kuwa taasisi. Slabolepszy akaboresha na kuanza kufanya kazi ya kutoa ripoti za michezo. Gazeti la eneo hilo lilipokea baadhi ya michango yake, hivyo akawa mwandishi wa habari wa michezo katika umri wa miaka 14.[1]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Simmonds, Ken. "ANTHONY AKERMAN AND PAUL SLABOLEPSZY IN CONVERSATION", SASWA, 18 April 2003. Retrieved on 2021-10-23. Archived from the original on 2007-09-20. 
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paul Slabolepszy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.