Ogopa Deejays
Ogopa Deejays |
---|
Ogopa Deejays ni timu ya kutengeneza na kurekodi muziki katika studio ya Kenya iliyoanzishwa mwisho wa miaka ya 1990 ambayo ilipata umaarufu katika kanda ya Afrika Mashariki kutokana na viwango vyake vya juu vya kutengeneza muziki.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Ogopa Deejays walianza kuwatengenezea wasanii kama vile Bebe Cool, Chameleon, Redsan na Nameless nyimbo motomoto. Ogopa Deejays wamedaiwa kwa upana kusaidia kukuza muziki wa Kenya wa kisasa kutoka kwa hali ya kutojulikana. Wao pia wanapongezwa kwa kuunda mtindo wa muziki wa Boomba (wakati mwingine muziki huu unafahamika kama Kapuka) ambao ni wa kisasa wa Kenya na ambao ni mchanganyiko wa “hip hop” na “Dancehall” uliyoshawishiwa na ngoma na midundo za Kiafrika. Baadaye wao walianzisha Ogopa Productions[1] ambayo haitengenezi muziki pekee lakini pia huandaa matukio.
Wametoa Albamu tatu ambazo zinajumuisha nyimbo za wanamuziki tofauti na Albamu kadhaa za wasanii wao. Albamu yao ya kwanza ilitolewa mwaka wa 2001 na ilikuwa maarufu sana katika kanda ya Afrika Mashariki. Pia wao ndiyo waliowaonyeha mashabiki talanta za marehemu E-Sir na K-Rupt. Wanajulikana sana na alama yao maarufu ya uso mwekundu unaopiga nduru.
Watu walioanzisha Ogopa DJ's ni mandugu Francis na Lucas Bikedo pamoja na meneja Banda. Nadra wao huonyesha nyuso zao hadharani na wao hukataa picha zao kuchukuliwa au kuchapishwa na vyombo vya habari vya Kenya.
Studio zao ziko katika mtaa wa South B mjini Nairobi. Wao pia wameanzisha studio nyingine katika nchi za Namibia na Afrika Kusini, inayojulikana kama Ogopa Butterfly. Wao wamewatengenezea muziki kundi la vipusa wawili wenye makao mjini Windhoek, Namibia wanaojulikana kama Gal Level na mwanamuziki Faizel MC ambaye anaasili ya Kikenya na Kinamibia.
Orodha ya wasanii wa Ogopa Deejays
[hariri | hariri chanzo]Orodha hii ni ya wasanii ambao wamesainiwa na Ogopa DJ's angalau wakati mmoja wa wasifu wao(wasanii ambao mara kwa mara wamerekodi na Ogopa wameondolewa):
- Amani
- Ngoni
- Big Pin
- Chameleone
- Nameless
- Juma Nature
- E-Sir
- Kleptomaniax
- K-Rupt
- Longombas
- Mr. Googz & Vinnie Banton
- Mr. Lenny & Kunguru
- Redsan
- Tattuu
- Wahu
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-16. Iliwekwa mnamo 2018-06-02.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ogopa Deejays Official Website Archived 8 Septemba 2010 at the Wayback Machine.
- Ogopa Butterfly Archived 8 Januari 2009 at the Wayback Machine.
- Mahojiano na DJ Edu Mahojiano ya BBC na DJ Edu kuhusu muziki wa Kenya.
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ogopa Deejays kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |