Redsan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Redsan (jina halisi: Swabri Mohammed; amezaliwa 1981) ni mwanamuziki wa reggae pamoja na ragga kutoka Kenya.

Albamu yake ya kwanza, "Seasons of the sun" ilitolewa mwaka 2002 chini ya Ogopa DJ's Nyimbo zilizojulikana kwenye albamu hiyo ni kama "Julie" na "Wanipa Raha".

Baadaye, alisajiri na Southwest Records, ambapo alitoa albamu yake ya pili,"Red" mnmamo mwaka wa 2004. Ilikuwa na nyimbo maarufu kama "Kuku" na "Apakatwe"[1]. Albamu yake ya tatu, Pioneer, ilitolewa mwaka wa 2006, na ilikuwa na nyimbo "Kenyan" na "Touch".

Redsan ameweza kuzuru mara kadhaa nchini Marekani na Ulaya.

Amewahi kushinda katika sehemu kadhaa katika Chaguo La Teeniez na pia Kisima Awards[2]. Katika Tanzania Music Awards ya 2006 albamu yake Pioneers iliteuliwa katika kiwango cha albamu bora Afrika Mashariki mnamo mwaka wa 2006 katika Pearl of Africa Music Awards alishinda katika sehemu ya Msanii bora mwanaume kutoka Kenya.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Redsan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.