Kleptomaniax

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kleptomaniax
Asili yake Nairobi, Kenya
Miaka ya kazi 1999-2010
Wanachama wa sasa
Roba
Collo
Nyashinski

Kleptomaniax ni kundi la kurap kutoka Nairobi, Kenya. Kundi hilo lina wanachama watatu: Roba (Robert Manyasa), Collo (Collins Majale) na Nyashinski (Nyamari Ongegu).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kleptomaniax ilianzishwa mwaka wa 1999, walipokuwa bado wanafunzi wa shule ya upili katika Shule ya Nairobi . Kundi hili lilijiunga na lebo ya Ogopa DJs na kutoa wimbo wao wa kwanza, "Freak It" mnamo 2002, ambao ulifuatiwa na "Maniax Anthem" na "Haree." [1] Mnamo 2004 kikundi kilitoa wimbo mwingine "Tuendelee", ambao umekua wimbo wao mkubwa hadi sasa. Wimbo huu uliandikwa kama jibu la " Diss track " na wanamuziki mbalimbali wa hip hop (ikiwa ni pamoja na Bamboo ), ambao walikosoa mtindo wa muziki wa Kapuka unaofanywa na Kleptomaniax . [2]

Albamu yao ya kwanza ya M4E (kifupi cha Maniax Forever ) ilitolewa mnamo 2005. Baadae mwaka huo kundi lilipokea uteuzi wa Tuzo za Muziki za MTV Ulaya kwa kipengele cha Best African Act, lakini tuzo hiyo alishinda msanii kutoka Nigeria 2Face Idibia . Mnamo 2007, Kleptomaniax walitembelea Marekani. [3] Kundi hilo lilisimamiwa na Fakii Liwali.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Daily Nation, Lifestyle Magazine, June 1, 2003: Kleptomaniax, the trio behind the hit songs
  2. The Standard, Pulse Magazine, April 25, 2005: Klepto’s beef with Pulse
  3. "Sambaza Entertainment". Sambazainc.com. 2007-02-24. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-17. Iliwekwa mnamo 2012-05-28. 
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kleptomaniax kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.