Wahu
Rosemary Wahu Kagwi, [1] anajulikana kitaaluma kwa jina moja la Wahu, ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Kenya, mwanamitindo wa zamani, mwigizaji na mjasiriamali.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa mwaka 1980 huko Nairobi. Wahu alisoma shule ya msingi ya Hospital Hill na kuendelea hadi shule ya upili ya Precious Blood mbayo iko Riruta . Akiwa shuleni, aliandika wimbo wake wa kwanza. [2] Wahu ni mwanamitindo wa zamani na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi, aliyehitimu shahada ya Sanaa katika hisabati na Mawasiliano .
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Alianza kazi yake ya muziki mnamo mwaka 2000. Alitoa wimbo wake wa kwanza "Niangalie" ambao ulipata mapokezi mazuri barani Afrika na duniani kote kwa ujumla. Nyimbo zake tatu za kwanza zilikuwa "Niangalie", "Esha" na "Liar". Wahu alitoa wimbo wake mkuu wa kwanza, "Sitishiki" karibu 2005. [3] Baadhi ya muziki wake umetayarishwa na ma DJ wa Ogopa . Wahu ameburudisha hadhira pamoja na Wasanii wengi wa Kenya na Afrika kama Kleptomaniacs, Fally Ipupa, Nonini, Nameless, Wyre, Qqu, na P-Unit . Yeye ndiye mpokeaji wa kwanza wa Tuzo za Muziki za MTV Afrika 2008, [4] kwa kitengo cha Msanii Bora wa Kike. Zaidi ya hayo, ameshinda Tuzo za Pearl of Africa Music Awards, Chaguo La Teeniez na Kisima Music Awards . [5] Katika tasnia ya uigizaji, Wahu alikuwa na nafasi kubwa katika kipindi cha televisheni cha Tazama
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Ameolewa na David Mathenge almaarufu Nameless, mwanamuziki mwingine wa Kenya. Wana watoto wa kike 2 wanaoitwa Tumiso na Nyakio. Alijitolea wimbo wake mkubwa zaidi hadi sasa "Sweet Love" kwa mmoja wa binti zake. [3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Wahu Kagwi". Ghafla. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-10. Iliwekwa mnamo 12 Januari 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kimani, Sheila. "#WCW: Wahu Kagwi - Of Music, Marriage and Motherhood". Standard Entertainment and Lifestyle (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-11-10.
- ↑ 3.0 3.1 "Despite lean season, Wahu bounces back". 21 Juni 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "MAMA Awards winners". Bella Naija. 23 Novemba 2008. Iliwekwa mnamo 12 Januari 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Kisima Awards Winners 2008/2009 announced!". I.fienipa. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 12 Januari 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wahu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |