Precious Blood Secondary School Riruta
Mandhari
Precious Blood Secondary School Riruta
Nchi | Kenya |
---|
Precious Blood Secondary School Riruta ni shule ya upili ya wasichana. Shule hii iko katika eneo la Nairobi, upande wa Kawangware.
Shule ya Precious Blood ni shule ya serikali, na inapata usaidizi wa Kanisa Katoliki.
Mavazi ya wanafunzi ni ya rangi ya kijani kibichi na nyeupe, na wanavaa viatu nyeusi.
Kwa miaka mingi, shule ya upili ya Precious Blood imepata matokeo bora kwenye mtihani wa KCSE. Mara nyingi shule hii huwa kati ya shule kumi ambazo zinaongoza nchi katika mtihani huu. Wasichana wa Precious Blood wameendelea kujiunganisha na Vyuo vikuu bora, Kenya na pia ng'ambo.