E-Sir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
E-Sir
Jina la kuzaliwa Issah Mmari
Pia anajulikana kama E-Sir
Amezaliwa 1981
Asili yake South C, Nairobi, Kenya
Aina ya muziki Hip hop, Kapuka
Kazi yake Rapa
Miaka ya kazi 2001-2003

Issah Mmari (20 Mei 1981) alikuwa msanii wa muziki wa hip hop na kapuka kutoka mjini Nairobi huko nchini Kenya. Alifahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama E-Sir. Alikuwa akifanyia shughuli zake katika studio ya Ogopa DJs ambaye alikuwa maarufu kwa uwezo wake wa kuimba na amri ya Kiswahili lugha. Bado yeye huonekana kama Muimbaji wa rap bora sana kuwahi kutokea nchini Kenya. Alikuja kujulikana mwaka 2001 na wimbo wakea wa "Jo", wimbo aliufanya katika sambamba na mtindo wa Black Rob katika ngoma yake ya "WHOA." Wimbo huo ulifanya E-Sir's ajulikane katika mziki wa Kenya na aliwekwa katika albamu ya Ogopa Deejays Aliweza kutoa alikwenda albamu yake ya "Nimefika" mwaka wa 2003 ambayo iliweza kufanya vema zaidi. Yeye alishinda katika sehemu 4 kwenya Kisima Music Awards.ya mwaka 2003

E-Sir alikufa katika ajali ya barabarani tarehe 16 Machi 2003, akiwa na mwenzake Nameless. Alikuwa njiani kutoka mji wa Nakuru ambapo alipokuwa ameenda kupigia upato albamu yake. Mashabiki wake walikuwa na huzuni na mshangao mkubwa baada ya kusikia juu ya msanii huyu shupavu. Hasaa hii ni kwa sababu kifo chake kilikuja wakati nyimbo zake zilikuwa zimeanza kufana sana nchini. Nyimbo zilizojulikana zaidi ni kama "Mos Mos," "Boomba Train," "Hamunitishi" na "Leo ni Leo." Kuna wimbo mmmoja uliotokea baada ya kifo chake.Wimbo huo alifanya na Nameless na unaitwa "Maisha".

Ndugu ya E-sir mdogo Habib pia ni msanii na pamoja na Manga wametoa nyimbo kadhaa kama"dunda" na "fever"

Albamu ya Nimefika[hariri | hariri chanzo]

Nyimbo kwenye Albamu

 • 1.Jobless corner 1 (Skit)
 • 2.Kamata
 • 3.Bamba
 • 4.Moss Moss
 • 5.Saree
 • 6.Jobless Corner 2 (skit)
 • 7.Sweet Kid ulimi twister
 • 8.Hamunitishi
 • 9.Deux Train
 • 10.Leo ni Leo
 • 11.Nimefika 'Jo'
 • 12.Saree
 • 13.Kamaiko (skit)

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Alishinda

 • Kisima Music Awards 2003 - Nyimbo ya mwaka ( "Bumba Train") & Mwanaume Mwanamziki wa mwaka, Albamu ya Mwaka ( "Nimefika")

Kuchaguliwa

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viunganish vya nje[hariri | hariri chanzo]