Nyama choma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nyama choma hotelini.
Nyama choma kwenye jiko dogo la makaa.

Nyama choma ni nyama iliyopikwa kwa kuchomwa kwa moto, makaa au jiko la umeme. Pia nyama inaweza kuchomwa na majiko maalum ya kisasa ya gesi ya kuchomea nyama.[1]

Nyama inaweza ama kuchomwa moja kwa moja, ama kwanza kuchemshwa au kupwikwa na moshi[2], mtindo maarufu hasa Marekani, kabla ya kuchomwa.

Harufu yake inavutia watu wengi kuipenda katika nchi na tamaduni mbalimbali duniani. Hivyo imekuwa biashara hasa katika barabara za mijini.

Nyama hii hupendwa pia wakati wa sherehe, matukio muhimu ya kifamilia na marafiki au mwisho wa wiki kwa wale wanaokunywa pombe. Pamoja na kuliwa na vyakula vingine, mara nyingi huandaliwa na kachumbari.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sharon Dempsey (10 July 2018). Buying Guide For The Best Gas Grills Under 500 (en-US). Guides Insider. Iliwekwa mnamo 12 July 2018.
  2. Muffin Group (2019-02-02). How To Smoke A Steak (en-US). Limited Red. Iliwekwa mnamo 2019-06-07.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyama choma kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.