Noor Bano (mwimbaji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Noor Bano (1942 - 14 Februari 1999) alikuwa mwimbaji kutoka Singh, Pakistan. Kwa sababu ya sauti yake nzuri na tamu, alikuwa maarufu mahali pote Sindh, hasa Singh vijijini.[1]

Biografia[hariri | hariri chanzo]

Noor Bano alizaliwa mnamo 1942 katika kijiji cha Mithoo Gopang karibu na Peero Lashari wilaya ya Badin Sindh. Baadaye alihamia Talhar Sindh. Jina la baba yake lilikuwa Suleman Gopang ambaye alikuwa mkulima maskini. Hakuhudhuria shule yoyote na alikuwa na kawaida ya kuimba nyimbo za harusi kwenye vijiji vilivyopo karibu.[2] Alipata mafunzo ya muziki kutoka kwa Hayat Gopang na Ustadhi Mithoo Kachhi.

Mwanachuoni mashuhuri Pir Ali Muhammad Shah Rashidi na Pir Hassamuddin Shah Rashidi walikuwa na mapenzi kwa muziki na utamaduni wa Sindh. Walitembelea makazi ya Syed Wadal Shah Rashidi huko Talhar. Syed Wadai Shah aliandaa programu ya muziki kwa heshima yao. Noor Bano aliitwa kuimba kwenye hiyo programu. Wageni walifurahiswa sana na sauti yake tamu asilia na walimshauri kuimba katika redio Pakistan Hyderabad. Pir Zaman Shah Rashidi, mtoto wa kiume wa Syed Wadal Shah alimtambulisha yeye katika Redio Pakistan mnamo mwaka 1960 mwishoni.[3] Wimbo wake wa kwanza katika Redio Pakistan ulikuwa “Munhnjay Marooaran joon boliyoon sujanan” (منهنجي ماروئڙن جون ٻوليون سڃاڻان). Wimbo huo ulidhihirisha kuwa mzuri na alikuwa maarufu katika kila kijiji cha Sindh. Wimbo wake mwingine mzuri ulikuwa "Munhinjay Mithran Marun Tay Ala Kakar Chhanwa Kajan". Mnamo 1970 na 1980 alikuwa miongoni mwa wanawake maarufu waimbaji wa nyimbo za kijadi huko Singh.

Kwenye Redio Pakistan, aliimba nyimbo nyingi kama mwimbaji wa kujitegemea, ingawa, pia aliimba pamoja na waimbaji maarufu Master Muhammad Ibrahim, Mithoo Kachhi, Zarina Baloch na Amina. Alikuwa pia maarufu kwa nyimbo zake za harusi za Kisingh zilizoitwa “Lada” au “Sahera”. Baadhi ya nyimbo zinapatikana katika maktaba ya Redio Pakistan Hyderabad.

Alikufa mnamo 14 Februari 1999 huko Talhar na alizikwa katika makaburi ya Hyder Shah Lakyari.[4] Mtoto wake wa kike Humaira Gopang alikuwa pia mwimbaji lakini hakupata mafanikio ya umaarufu kama wa mama yake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-13. Iliwekwa mnamo 2021-04-13. 
  2. Rahookro Usman; Noor Bano Gopang, Sona Sarekhiyoon Sartiyoon (In Sindhi), pp. 145, Samroti Publication, Tharparker, 2017.
  3. "Mai Noor Bano Sindhi Folk Music Singer". Media Music Mania (kwa en-US). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-05-19. Iliwekwa mnamo 2020-04-13.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  4. Chandio, Khadim Hussain; Noor Bano, Maroo Jay Malir Ja (in Sindhi), pp. 242, Ganj Bux Kitab Ghar, 2002.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Noor Bano (mwimbaji) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.