Nnenna Okore

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nnenna Okore

Amezaliwa 1975
Australia
Nchi Australia
Kazi yake Msanii

Nnenna Okore (alizaliwa Australia, 1975) ni msanii anayefanya kazi zake nchini Nigeria na Marekani. Kazi zake nyingi zinahamasishwa na muundo, rangi na fomu zinazomzunguka.[1] Kazi nyingi za Okore hutumia Flotsam, jetsam, lagan, na derelict au maombo yaliyozuiliwa ili kutengeneza mandhari na picha ya matumizi mengi ya nguvu kazi ya mwanadamu.[2] Alijifunza baadhi ya mbinu zake kama kushona, kushikisha, kubadili rangi na kusokota,[3] kwa kutazama namna watu wa kawaida wanavyofanya shughuli zao za kila siku.[2][4] Kazi nying za Okore huchunguza safu zenye vielelezo vingi, na kazi zake zimekua zikionyeshwa katika makumbusho na maonyesho mbalimbali ndani na nje ya Marekani.[2][3][5][6] Ameshinda tuzo za kimataifa, mojawapo ni ‘’Fulbright Scholar Award’’ mwaka 2012.[7]

Okore kwa sasa ni mhadhiri wa chuo kikuu cha North Park ‘’North Park University’’ jijini Chicago, ambamo atafundisha Sanaa ya sanamu.[8]Binti wa proffesa na mkutubi hua mara kwa mara anatathmini utambulisho wake kama mmarekani na kuulinganisha na utambulisho wake kama mnigeria na hueleza utofauti kati ya mahala alipozaliwa na Marekani.[2]

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Okore alizaliwa visiwa vya Thursday Island, nchini Australia, wazazi wake ni watu wa Ututu, Jimbo la Abia nchini Nigeria.[9][10] Aliporudi nchini Nigeria akiwa na umri wa miaka minne, Okore alitumia muda wake mwingi katika mji wa Nsukka uliopo kusini mashariki mwa Nigeria, wazazi wake wote walikua ni wakufunzi katika chuo kikuu cha Nigeria.[9] Sanaa ya Okore iliathiriwa san ana mandhari ya Nsukka, kama vile uwepo wa nyumba zilizojengwa kwa tope zikiwa na mabati ya kisasa, mrundikano wa kuni pembezoni mwa jingo lililovunjwa, watu katika mavazi chakavu na mandhari chakavu.

Akiwa anaishi katika makazi ya wakuu, yaliyokuwa karibu na mipaka ya chuo, Okore mara nyingi aliweza kunana na wakazi ambao sio wafanyakazi wa ndani ya chuo, aliweza kutambua masoko ya karibu Pamoja na kukutana na wakazi wengi wa maeneo ya mijini. Leo hii, kazi yake imelenga matumizi ya vifaa asilia kama vile ufinyanzi, kama, nyuzi, vijiti na karatasi ambavyo alikua anakutana navyo kila mara wakati akiishi Nsukka.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Okore alipata elimu yake ya msingi na sekondari kutoka shule inayomilikiwa na chuo kikuu cha Nigeria, Baadaye alijiunga na shule ya upili ya Waterford (‘’Waterford Kamhlaba United World College’’) nchini [[[Swaziland]]. Alipenda sana masuala ya Sanaa alipokua shule ya msingi, alipenda kushona, kufuma na kupandikiza. Wakati huo, Okore alishinda tuzi nyongi za Sanaa, mojawapo ni ya UNESCO katika mashindano ya sanaa ya Watoto barani Afrika mwaka 1993. Akiwa sekondari, alipendelea zaidi sanaa ya uchoraji na kupaka rangi. Familia yake, hasahasa baba yake bwana A. O. Okore, walimpa ushirikiano na kumuunga mkono kwa asilimia kubwa, wakimtia moyo katika ndoto zake za kuwa msanii.

Alipohitimu kutoka shule ya upili huko nchini Swaziland, Okore alikua mahiri katika sanaa ya uchoraji, ufinyanzi na uchapishaji. Miaka michache baadae, alipata tuzo ya UNIFEM ashindano ya tuzo za kuwawezesha wanawake, zawadi zilizohusishwa ni Pamoja na safari ya kwenda Dakar, Senegal; Abuja, Nigeria; na Beijing, China, kama muwakilishi wa wanawake katika tamasha la wanawake la ulimwengu.

Mwaka 1995, Okore alijiunga na chuo kikuu cha Nigeria kwa masomo ya Sanaa. Kazi zake za awali zilihusisha kupaka rangi za mafuta. Akiwa mwaka wa tatu, Okore alianza kutafiti juu ya matumizi ya vitu ambavyo sio vya kawaida katita tasnia ya upakaji rangi kama vile matumizi ya canvas, hii ikiwa ni jitihada za kutofautisha kazi zake na wasanii wengine. Alitumi majani, nguo, vijiti, picha chakavu na karatasi. Okore alipata hamasa kuto kwa walimu wake wakiwemo, Chijioke Onuora, Chike Aniakor, na El Anatsui. Okore alipata shahada ya sanaa kutoka chuo kikuu cha Nigeria mwaka 1999, akiwa na ufaulu wa juu kabisa wa heshma.

Miaka miwili baadaye, Okore alihamia nchini Marekani kwa ajili ya masomo ya Uzamili katika sanaa huko chuo kikuu cha Iowa, ambapo alihitimu mwaka 2005.[7]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu cha Iowa, Okere alipata ajira kutoka chu kikuu cha North Park kufundisha na kusimamia idara ya sanaa. Kwa sasa anafanya kazi kama mkufunzi na mkuu wa idara, akielekeza wanafunzi wa shahada katika Nyanja tatu, uchoraji, uchongaji sanamu na matengezo ya maombo yenye pande tatu.[7]

Pamoja na kazi yake ya ukufunzi, kazi za Okore zimekua zikionyeshwa sehemu mbalimbali ulimwenguni katika makumbusho na hadhira mbalimbali katika mabara ya Asia, Ulaya, Marekani ya kaskazini na Afrika. Kazi zake zimekua zikielezewa kwa namna ya kipekee kwatika majrida kama vile Sculpture Magazine, The New York Times, Financial Times, Art South Africa na Ceramics: Art and Perception. Alifanya maonyesho yake ya kwanza mwaka 2001 yenye jina la ‘’Metaphors’’ jijini Lagos, Nigeria. Maonyesho yake ya pili yalikwenda kwa jina la ‘’Beyond the lines’’ katika makumbusho ya Didi, Lagos Nigeria mwaka 2002. Alifanya maonyesho yake binafsi ya kwanza nchini Marekani mwaka 2002 na kulipa jina la ‘’Re-presented’’ huko chu kikuu cha Iowa. Tangu hapo, amekua akifanya maonyesho ya aina hii kila mwaka.[11]

Mwaka 2012, Okore alpata tuzo kwa jina ‘’Fulbright Scholar Award’’. Iliambatana na ruzuku, alisafiri kwenda Nigeria katika kazi ya ukufunzi katika chuo kikuu cha Lagos, ambamo aliendele na uzalishaji wa kazi za sanaa na ubunifu wa hali ya juu. Baadaye baada ya kumaliza kazi hiyo, alirejea nchini Marekani mwaka 2013.

Nyenzo[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni mwa Maisha ya Okore akiwa nchini Marekani, alionekana mwenye utofauti mkubwa sana wa kimazingira na utamaduni. Akiwa bado anajaribu kuingia katika mazingira ya huko, aliendelea na matumizi ya vifaa ambavyo alikua anatumia alipokua nchini kwake.

Okore anapendelea matumizi ya vitu asilia. Katika kazi zake za hivi karibuni, vifaa vyake vimeweza kuonyesha matumizi ya vifaa vinavyopatikana kwa urahisi. Matumizi ya karatasi yaeweza kumpatia njia tofauti tofauti za kufanya kazi zake.

Maonyesho ya sanaa[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nnenna Okore kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.