Nenda kwa yaliyomo

São Paulo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa São Paulo

São Paulo (Kireno: Mt. Paulo) ni jiji kubwa la Brazil pia jiji kubwa katika nusudunia ya kusini lenye wakazi zaidi ya milioni 10 jijini au karibu milioni 20 katika rundiko la jiji.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1554 mapadre wawili Manuel da Nóbrega na Yosefu wa Anchieta walijenga kituo cha misioni pamoja na shule kwa kuwalengea wenyeji asilia wa Brazil.

Kituo kiki kilikuwa mbegu wa kijiji, baadaye mji (1711) halafu jiji la Mt. Paulo.

Wakati wa karne ya 18 kilimo cha sukari kiliimarisha kilimo cha eneo la mji. Karne ya 19 ilileta kilimo cha kahawa na wahamiaji wengi kutoka Ulaya hasa kutoka Italia. Katika karne ya 20 viwanda viliongezeka.

Leo hii jiji ni kitovu cha biashara, huduma na teknolojia cha Brazil yote.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Rundiko la jiji la Sao Pauli (nyekundu)
mitaa ya São Paulo

São Paulo iko katika nyanda za juu kwenye kimo cha 760 m juu ya UB. Hali ya hewa ni ya kupoa.

Kuna uwanja wa ndege tatu. Barabara maarufu mno ni Avenida Paulista.

Makala hii kuhusu maeneo ya Brazil bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu São Paulo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.