Nenda kwa yaliyomo

Njacko Backo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Njacko Backo

Njacko Backo ni mwanamuziki, mshahiri, mwandishi,mtumbuizaji,mtunzi na mwalimu wa dansi kutoka Kamerun. Alizaliwa 1958 na kulelewa katika familia ya wanamuziki.[1] Alitumia muda wake mwingi wa utotoni katika kijiji cha Bazou magharibi mwa Kamerun ambapo alitambulishwa kwenye muziki. Kama watoto wengi katika kijiji chake, alianza kucheza kibati na kutengeneza vifaa. Kwa msaada wa bibi yake, Njacko alikutana na wakuu wa kijiji waliomfundisha namna ya kucheza muziki.Alijifunza ngoma, Kalimba, Kibati na zaa koua.

Maisha Binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Njacko aliondoka Kamerun akiwa na umri wa miaka 17.[2] na kuendelea kusoma muziki wa kisasa na wa kitamaduni wa kiafrika wakati aliposafiri katika nchi za Afrika ya kati na Magharibi ambazo baadhi ni Nigeria, Benin, Togo, Ghana, Ivory Coast, Burkina Faso, Senegal, Niger na Mali. Wakati akiishi Ulaya, Njacko aliendelea kufanya kazi kama mwanamuziki, mchezaji dansi na mwalimu wa dansi na kufanya kazi na vikundi kama vile Africa Salimata, Ernest Cissé, Sosoba, Vinjama na Mioso Mika.[3]

Kwa sasa Njacko anaishi Toronto,Ontario, Canada ila awali alifikia Montréal Quebec mwaka 1989.Alifanya kazi pamoja na wanamuziki wengine wa kiafrika akiwemo hayati Boubacar Diabaté, Oumar Diayé, na mcheza dansi Zab Maboungou. Aliunda bendi yake Njacko Backo na Kalimba Kalimba mwaka 1990 na amekwisha toa albamu 11 mpaka sasa. Njacko Backo alitumbuiza katika tamasha la Montreal, Louisiana Folk na Houston International Jazz ambazo ni miongoni mwa matamasha nyingi alizozifanya. Pia amekwisha tunga muziki kwa ajili ya filamu ikiwemo filamu kama To Walk with Lions, Born Free na Spirit in the Tree.

Ukiachilia mbali muziki, Njacko anafundisha katika eneo la Toronto kupitia shirika linaloitwa Mariaposa.[4]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Njacko Backo Biography". Black In Canada (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-05-17. Iliwekwa mnamo 2019-11-21. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  2. "Artist Profiles: Njacko Backo | World Music Central.org" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-11-21.
  3. "The More You Read: Los Angeles Actor & Writer, Clark Backo's IGTV series & Podcast" Archived 20 Mei 2022 at the Wayback Machine.. Collective Culture, July 2020.
  4. "Our Artists". Mariposa in the School. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo Novemba 13, 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Njacko Backo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.