Nindai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Nindai ni kijiji kilichopo katika mwambao wa Ziwa Nyasa. Kijiji hiki kimepakana na vijiji vya Tawi, Yola na Nambingi. Kijiji kiko katika kata ya Ngumbo, Wilaya ya Nyasa.

Mzee Magerumani ni mmoja wa waasisi wa kijiji hiki toka katika koo za kina Sekamaganga na kina Nchimbi. Parokia yao ni Mango Mission.

Hospitali waitumiayo iko Litembo katika wilaya ya Mbinga.

Kijiji hiki husifika sana kwa uvuvi wa dagaa na samaki. Baada ya operesheni vijiji kijiji kilibadilishwa jina na kuitwa Liundi ambako kuna shule ya msingi kandokando ya milima ya Livingstone na mto Miche ambao humwaga maji ziwani Nyasa.

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Nyasa - Mkoa wa Ruvuma - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Chiwanda | Kihagara | Kilosa | Kingerikiti | Linga | Liparamba | Lipingo | Lituhi | Liuli | Liwundi | Luhangarasi | Lumeme | Mbaha | Mbambabay | Mipotopoto | Mpepo | Mtipwili | Ngumbo | Tingi | Upolo