Ndezi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ndezi
Ndezi mkubwa (Thryonomys swinderianus)
Ndezi mkubwa (Thryonomys swinderianus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wagugunaji)
Nusuoda: Hystricomorpha (Wanyama kama nungunungu)
Familia: Thryonomyidae (Wanyama walio na mnasaba na ndezi)
Pocock, 1922
Jenasi: Thryonomys
Fitzinger, 1867
Ngazi za chini

Spishi 2:

Ndezi ni wagugunaji wakubwa wa familia Thryonomyidae ambao wana mnasaba karibu kiasi na nungunungu. Wanatokea mahali panyevu pa Afrika kusini kwa Sahara. Wamo miongoni mwa wagugunaji kubwa kabisa duniani. Mwili wao una urefu wa sm 35-60 na uzito wa kg 6-10. Wana manyoya magumu yenye rangi ya kahawa na vidoa kijivu na njano. Hula manyasi ya maji porini lakini katika maeneo ya kilimo hula mimea ya shamba kama muwa, muhogo n.k. Wanaweza kudidimiza hasara kubwa. Ndezi hufugwa sana huko Benini na Togo, na hata nchini Kameruni, Kodivaa, Gaboni, Gana, Nijeria, Senegali na Kongo wakulima wahimizwa kufuga wanyama hawa. Nyama yao ni nzuri sana.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]