Namba ya simu ya bure

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Namba ya simu ya bure ni namba ya simu ambayo malipo yake ni jukumu la mpokeaji simu na sio yule anayepiga.

Mfumo huu ambao hutumia namba 800, 0800 au 1-800 unatumiwa katika nchi mbalimbali duniani kama vile Marekani, Australia, Pakistani, Uingereza, Uholanzi, Kanada, n.k.

Huko nyuma, simu kupitia namba hizi zikikuwa lazima zipokelewe kwanza na mfanyakazi wa kampuni ya simu. Mfanyakazi huyu alitakiwa kupata ruhusa toka kwa anayepigiwa simu kabla ya kumuunganisha na mpigaji simu. Maendeleo ya teknolojia ya digitali yamebadilisha mfumo huu. Mpigaji simu hivi sasa akipiga simu inakwenda moja kwa moja bila kupitia kwa mtumishi wa kampuni ya simu. Kabla ya mwaka 2015, namba hizi hazikuwa bure kwa watumiaji wa simu ya mkononi. Hivi sasa hata watumiaji wa simu ya mkononi wanaweza kupiga namba hizi bila gharama yoyote.

Namba hizi hutumiwa sana na makampuni makubwa na idara mbalimbali za serikali.

Mifano mbalimbali duniani[hariri | hariri chanzo]

  • Ajentina hutumia "0800" ikifuatiwa na tarakimu 7.
  • Armenia hutumia "800" ikifuatiwa na tarakimu 5.
  • Australia hutumia "1800", "1300", "13" ikifuatiwa na tarakimu 4 hadi 10.
  • Azerbaijani hutumia 088 ikifuatiwa na tarakimu 7.
  • Ubelgiji hutumia "0800" ikifuatiwa na tarakimu 5
  • Brazili hutumia "0800" ikifuatiwa na tarakimu 7

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]