Nenda kwa yaliyomo

Mwingasiafu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwingasiafu
(Canavalia ensiformis)
Mwingasiafu unaobeba kaka
Mwingasiafu unaobeba kaka
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Nusufamilia: Faboideae (Mimea inayofanana na mharagwe)
Jenasi: Canavalia
DC.
Spishi: C. ensiformis
(L.) DC.

Mwingasiafu (Canavalia ensiformis) ni mmea wa mazao wa nusufamilia Faboideae katika familia Fabaceae. Huitwa mpupu pia lakini tafadhali jina hili litengewe Mucuna pruriens (mpupu). Spishi hii hufananishwa mara nyingi na mbwanda (C. gladiata) lakini maua ni pinki na makaka ni marefu sana (hadi sm 36). Makaka na mbegu huitwa bwanda kama zile za C. gladiata.

Mwingasiafu hukuzwa katika Afrika ya Mashariki kama zao la kufunikia na matandazo kijani. Makaka mabichi na mbegu mbichi zinaweza kuliwa lakini lazima zipikwe vizuri ili kutoa sumu zao. Mimea inaweza kutumiwa kama malisho lakini lazima isichanganywe na urea, kwa sababu ina kima kikubwa cha kimeng'enya urease ndani yao kinachotoa ammonia yenye madhara. Pia mbegu mbivu zinaweza kuliga wanyama zikiwa nyingi sana.

Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwingasiafu kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.