Mbwanda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mbwanda
(Canavalia gladiata)
Mibwanda
Mibwanda
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Nusufamilia: Faboideae (Mimea inayofanana na mharagwe)
Jenasi: Canavalia
DC.
Spishi: C. gladiata
(Jacq.) DC.

Mbwanda, mbwende au mkwende (Canavalia gladiata) ni mmea wa mazao wa nusufamilia Faboideae katika familia Fabaceae. Mbegu zake, zinazoitwa bwanda au bwende, zinakua ndani ya makaka yanayofanana na upanga. Hata makaka huitwa bwanda. Spishi nyingine za jenasi Canavalia hufananishwa mara nyingi na mbwanda, k.m. C. cathartica (mtela), C. ensiformis (mwingasiafu) na C. rosea (mgobi). C. africana na C. gladiata zinaweza kuwa spishi moja tu na mbile zote huitwa mbwanda.

Mbwanda hukuzwa katika nchi mbalimbali za Afrika, k.m. Madagaska na Tanzania (“kula bwanda” = kufurahi). Makaka mabichi na mbegu mbichi hulika. Lakini mbegu mbivu zina sumu, kwa hivyo lazima zipikwe vizuri na ganda la mbegu litolewe.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbwanda kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.