Mwanangu Rudi Nyumbani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwanangu Rudi Nyumbani ni kitabu cha tungo za mashairi (Diwani) chenye kuzungumzia mambo mbalimbali ya kijamii kupitia fasihi andishi ya Kiswahili.[1]

Kitabu hicho ni muswada wa tungo iliyojinyakulia ushindi wa Tuzo ya Mabati Cornell mwaka 2017 baada ya kusomwa na majaji watatu ambao ni Ken Walibora, Daulat Abdallah Saidi pamoja na Ali Attas

Mwanangu Rudi Nyumbani [2] ni shairi lilobeba jina la diwani hii, likiwa ni shairi la mama kumsisitiza mtoto wake arudi nyumbani ili ajishughulishe na kilimo kwani mji wa Mzizima hauwezi kutokana na tabu nyingi zikiwemo wizi, miundombinu mibaya ambayo si salama kwa mtoto wake, msongamano wa magari.

Mama pia, kupitia njia ya simu, anaendelea kumwambia mtoto wake jinsi anavyoumia kwa yeye kukosa kazi.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Mwanangu Rudi Nyumbani (en-US). Mkuki na Nyota Publishers (2018-12-12). Iliwekwa mnamo 2020-02-08.
  2. Rangimoto, Dotto.. Mwanangu rudi nyumbani. ISBN 978-9987-08-374-9. OCLC 1104922726. 
Books-aj.svg aj ashton 01.svg Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanangu Rudi Nyumbani kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.