Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Moongateclimber/Sandbox

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Muziki wa dansi (au dansi tu) ni muziki kutoka nchiniTanzania. Ulianzishwa katika mji wa Dar es Salaam kunako miaka ya 1930, na unapendeka leo hadi leo hii. Muziki wa dansi unatokana na muziki wa soukous kutoka Kongo-Kinshasa (au "rumba ya kikongo") na tokea hapo ikawa inaitwa "rumba ya Tanzania" pia. Kwa kawaida, maneno ya nyimbo ya muziki wa dansi ni kwa lugha ya Kiswahili; tokea hapo awali na pia dansi huitwa "swahili jazz" kwa lugha ya Kiingereza.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Muziki ulianzishwa kunako miaka ya 1920-1930, zikiwa na mandhari ya muziki wa "soukous" kutoka Kongo-Kinshasa, kwa kweli zilipendeka kote Afrika ya Mashariki. Katika Dar es Salaam, bendi nyingi zilifuatisha bendi za Kongo. Punde kwa punde, zingine ziliendeleza kuanzisha mitindo mipya, kwa mfano Dar es Salaam Jazz Band, Morogoro Jazz na Tabora Jazz.

Baada ya uhuru wa Tanzania, bendi nyingi za muziki wa dansi nilitegemea ofisi au vyama. Kwa mfano, NUTA Jazz Band ilikuwa bendi bayana na ilitegemea Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania ("National Union of Tanzania", NUTA, kwa Kiingereza).

Kunako miaka ya 1960-1980 muziki wa dansi uliendelea kwa ajili ya bendi bayana kama Orchestra Safari Sound, Orchestra Maquis Original, International Orchestra Safari Sound, DCC Mlimani Park Orchestra na Vijana Jazz. Baadhi ya bendi kisasa ni Gari Kubwa, Tokyo Ngma na Atomic Advantage.

Bendi nyingi za muziki wa dansi zilicharaza kila usiku, katika vilabu, mahoteli na kadhalika, na wanamuziki walipokezana. Kwa mfano Morogoro Jazz ilicharaza katika hoteli ya "Morogoro Hotel" ya Morogoro. Pia wanamuziki walikuwa wakifanyakazi kwa kulipwa, na bendi ilikuwa imikimiliki vyombo vya muziki. Wanamuziki mashuuri walibadili bendi mara nyingi, hata kuchuma zaidi na hatimaye kuanzilisha bendi zao. Kwa mfano Muhiddin Maalin na Hassani Bitchuka walicharaza katika mabendi mengi.

Kila bendi huwa na mtindo unatambulikana, na mwanamuziki hujikaribisha kwa mtindo wa bendi yao baada ya kuajiriwa. Kwa kawaida jina la mtindo larejea gungu, kwa mfano ogelea piga mbizi ya Orchestra Maquis Original. Wasanii wengine hujulikana kwa sababu huweza kuunda mitindo vizuri.

Kwa kawaida, nyimbo wa muziki wa dansi huanza polepole kusisitiza maneno na mwimbaji; kisha, hatua kwa hatua hukuwa haraka (kipande hiki huiitwa chemko), na ngoma na magitaa huongeza kwa sauti.

Ushindani baina ya bendi kubwa ni muhimu kwa muziki wa dansi. Kwa mfano, Orchestra Maquis Original hushindana na Orchestra Safari Sound (kunako miaka ya 1970-1980) na baadaye International Orchestra Safari Sound hushindana na Mlimani Park. Sherehe za muziki wa dansi hufanywa kama shindano pia.

Bendi kubwa

[hariri | hariri chanzo]
Bendi Majina mengine Wakati Mji Mitindo mashuhuri Wanamuziki mashuhuri
Dar es Salaam Jazz Band Dar Jazz miaka ya 1930-1970 Dar es Salaam Michael Enoch
Morogoro Jazz Band Morogoro Mbaraka Mwinshehe, Salim Adballah
NUTA Jazz Band Juwata Jazz Band, OTTU Jazz Band miaka ya 1960-leo Joseph Lusungu, Mnenge Ramadhani, Muhiddin Maalim, Hassani Bitchuka, Saidi Mabera, Abel Balthazar
Orchestra Maquis Original miaka ya 1970-leo Dar es Salaam ogelea piga mbizi, kamanyola, zembwela Chinyama Chianza, Nguza Mbangu, Dekula Kahanga
Orchestra Safari Sound miaka ya 1970-1985 Ndala Kasheba
Mlimani Park Orchestra 1978-? sikinde Muhiddin Maalim, Hassani Bitchuka, Abel Balthazar, Michael Enoch, Cosmas Chidumule, Shaaban Dede
Vijana Jazz miaka ya 1980-1990
International Orchestra Safari Sound IOSS 1985-? ndekule Muhiddin Maalim, Hassani Bitchuka, Abel Balthazar, Nguza Mbangu

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]