Nenda kwa yaliyomo

Mtibwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mtibwa ni kata ya tarafa ya Turiani, Wilaya ya Mvomero katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi namba 67304.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 38,287 [1].Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 31,382 [2] walioishi humo.

Mtibwa iko katika eneo la mashamba makubwa ya miwa kwenye bonde la mto Mvomero yanayomilikiwa na kampuni ya Mtibwa Sugar Estates Ltd. inayomiliki hapa hektari 6,000[3] na kuajiri zaidi ya watu 3,000 wakati wa mavuno[4].

Pamoja na tasnia ya sukari Mtibwa / Turiani ni pia nyumbani kwa Mtibwa Sugar F.C. inayocheza katika ligi ya kitaifa ya Tanzania.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Morogoro - Mvomero DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-06-04.
  3. Viwanda, tovuti ya Bodi ya Sukari Tanzania, iliangaliwa Desemba 2019
  4. Takwimu za ajira -Peak employment,tovuti ya Bodi ya Sukari Tanzania, iliangaliwa Desemba 2019
Kata za Wilaya ya Mvomero - Mkoa wa Morogoro - Tanzania

Bunduki | Dakawa | Diongoya | Doma | Hembeti | Homboza | Kanga | Kibati | Kikeo | Kinda | Kweuma | Langali | Luale | Lubungo | Mangae | Maskati | Melela | Mgeta | Mhonda | Mkindo | Mlali | Msongozi | Mtibwa | Mvomero | Mziha | Mzumbe | Nyandira | Pemba | Sungaji | Tchenzema


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mtibwa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.