Nyandira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyandira ni mojawapo ya kata zilizopo katika wilaya ya Mvomero, mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67323.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 7,801 [1].

Katika kata hii wakazi walio wengi ni Waluguru. Upande wa dini, wengi wao ni Wakristo wa Kanisa Katoliki.

Wakazi wa eneo hili wanashughulika zaidi na kilimo, biashara, ufugaji na elimu. Zaidi sana wakazi wa kata hii wanashughulika na masuala ya utamaduni, kwa mfano, ngoma za asili kama vile mbeta, chikudindi, ritutu, chibwiko n.k.

Kata hii ina vijiji na vitongoji mbalimbali, vikiwemo: Chogo, Mtamba, Mhvisomi, Magana, Lubwe,kibuko Vidigisi, Ndughutu, Msewe, Tawa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Mvomero - Mkoa wa Morogoro - Tanzania

Bunduki | Dakawa | Diongoya | Doma | Hembeti | Homboza | Kanga | Kibati | Kikeo | Kinda | Kweuma | Langali | Luale | Lubungo | Mangae | Maskati | Melela | Mgeta | Mhonda | Mkindo | Mlali | Msongozi | Mtibwa | Mvomero | Mziha | Mzumbe | Nyandira | Pemba | Sungaji | Tchenzema


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyandira kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.