Nenda kwa yaliyomo

Mkindo (Mvomero)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mkindo ni kata ya Wilaya ya Mvomero katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania.

Mkindo kilikuwa kijiji cha kata ya Hembeti. Kwa sasa kijiji cha Mkindo ni kata mpya baada ya kata ya Hembeti kugawiwa. Kijiji cha Mkindo nacho kikagawanyika na kuzaa Bungoma. Hivyo kata ya Mkindo ina vijiji vinne ambavyo ni Mkindo, Kambala, Mndela na Bungoma.

Kijiji cha Mkindo kina vitongoji vitatu ambavyo ni Gulioni, Bugumo na Kilanga wageni.

Kijiji hiki kina jumla ya shule za msingi mbili. Shule ya msingi Mkindo A na Shule ya msingi Mkindo B. Pia kina zahanati moja na gulio (soko la wiki) ambalo hufanyika kila Jumamosi.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 15,523 [1].

Shughuli kubwa ya wakazi wake ni uvuvi pamoja na kilimo cha mazao makuu ya mpunga na mahindi.

Kuna bonde kubwa la mpunga ambalo ni maarufu sana, linaitwa Mgongola. Pia wananchi wanajishughulisha na kilimo cha umwagiliaji katika shamba linaloitwa SIDU.

Kata za Wilaya ya Mvomero - Mkoa wa Morogoro - Tanzania

Bunduki | Dakawa | Diongoya | Doma | Hembeti | Homboza | Kanga | Kibati | Kikeo | Kinda | Kweuma | Langali | Luale | Lubungo | Mangae | Maskati | Melela | Mgeta | Mhonda | Mkindo | Mlali | Msongozi | Mtibwa | Mvomero | Mziha | Mzumbe | Nyandira | Pemba | Sungaji | Tchenzema


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkindo (Mvomero) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.