Mbadili jinsia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Msenge)

Wabadili jinsia (Kiingereza: transgender people) ni aina ya watu ambao hujisikia, hujifikiria na kujiona au kujiigiza tofauti na jinsia zao za kuzaliwa nazo.

Pia kuna wale wanaoitwa kwa Kiingereza Transsexual: hawa ni miongoni mwa watu waliozaliwa na jinsia ya kiume wakataka wafanyiwe upasuaji ili wawe kama wanawake au kinyume chake. Mara nyingi wanaume ndio hutaka kuwa na viungo kama vya kike. Hata hivyo hadi sasa jinsia haiwezi kubadilishwa. Matumizi ya mfululizo ya homoni na upasuaji katika viungo vya uzazi unaishia upande wa nje bila kubadili wala kuathiri DNA ya mhusika.

Wabadili jinsia huwa wanafariki dunia mapema kuliko watu wengine,[1] pengine kwa kujiua, pengine kwa sababu ya kubaguliwa katika baadhi ya mazingira [2][3][4][5], lakini si kwa sababu hiyo tu. Tafiti mbalimbali zimeonyesha watu hao wana matatizo makubwa ya kiakili. [6] [7][8]

Kwa mujibu wa jumla ya tafiti zilizopima majuto ya wabadili jinsia, asilimia 1 ya wabadili jinsia wamarekani wanajuta kubadili jinsia[9]. Asilimia 10 za wabadili jinsia wamarekani waliacha kubadili jinsia.[10][11] Miongoni mwa wale walioacha, asilimia 62 walirudia kubadili jinsia yao na sasa wanabadili jinsia yao tena.[10] Sababu zao za kuacha kujibadilisha ni mbalimbali, lakini sababu ya kawaida sana ni hofu ya ubaguzi na kukanwa na jamii.[11]

Baadhi ya waliojuta wamefungua kesi dhidi ya waliowaelekeza, hasa baada ya kuona ugumu mkubwa wa kurudia hali asili (jambo ambalo pengine haliwezekani kabisa, hasa upande wa uzazi). Vilevile baadhi ya wazazi wao.

Dawa za kubadilisha jinsia zinaboresha afya ya akili ya wabadili jinsia wengi.[12] Lakini, dawa hizo pia zinaweza kuwa na athiri mbaya kwa watu wengine.[13]

Tazama pia

Marejeo

 1. https://www.hcplive.com/view/mortality-rate-higher-transgender-people
 2. Perez-Brumer, Amaya; Day, Jack K.; Russell, Stephen T.; Hatzenbuehler, Mark L. (2017-09-01). "Prevalence and Correlates of Suicidal Ideation Among Transgender Youth in California: Findings From a Representative, Population-Based Sample of High School Students". Journal of the American Academy of Child & Adolescent Psychiatry 56 (9): 739–746. ISSN 0890-8567. PMC 5695881 Check |pmc= value (help). PMID 28838578. doi:10.1016/j.jaac.2017.06.010. 
 3. Seelman, Kristie L. (2016-10-02). "Transgender Adults' Access to College Bathrooms and Housing and the Relationship to Suicidality". Journal of Homosexuality 63 (10): 1378–1399. ISSN 0091-8369. PMID 26914181. doi:10.1080/00918369.2016.1157998.  Unknown parameter |s2cid= ignored (help)
 4. Bauer, Greta R.; Scheim, Ayden I.; Pyne, Jake; Travers, Robb; Hammond, Rebecca (2015-06-02). "Intervenable factors associated with suicide risk in transgender persons: a respondent driven sampling study in Ontario, Canada". BMC Public Health 15 (1): 525. ISSN 1471-2458. PMC 4450977. PMID 26032733. doi:10.1186/s12889-015-1867-2. 
 5. Cohen-Kettenis, Peggy T.; Doreleijers, Theo A. H.; Wagenaar, Eva C. F.; Steensma, Thomas D.; McGuire, Jenifer K.; Vries, Annelou L. C. de (2014-10-01). "Young Adult Psychological Outcome After Puberty Suppression and Gender Reassignment". Pediatrics (kwa Kiingereza) 134 (4): 696–704. ISSN 0031-4005. PMID 25201798. doi:10.1542/peds.2013-2958.  Unknown parameter |s2cid= ignored (help)
 6. McNeil, Jay; Bailey, Louis; Ellis, Sonja; Morton, James; Regan, Maeve; Scottish Transgender Alliance; TREC; Traverse: Crossing Boundaries in Research; Sheffield Hallam University; TransBareAll (September 2012). "Trans Mental Health Study 2012". .gires.org.uk. Multiple. Iliwekwa mnamo 20 December 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
 7. Transgender Equality Network Ireland (TENI) (2 December 2013). Press Release: New survey reveals nearly 80% of trans people have considered suicide (Press release). Transgender Equality Network Ireland (TENI). Archived from the original on 5 March 2016. https://web.archive.org/web/20160305071910/http://teni.ie/news-post.aspx?contentid=970. Retrieved 20 December 2014.
 8. https://www.lifesitenews.com/analysis/mainstream-media-downplays-alarming-rates-of-depression-suicidality-among-gender-confused-teens/?utm_source=digest-profamily-2023-02-22&utm_medium=email
 9. Bustos, Valeria P.; Bustos, Samyd S.; Mascaro, Andres; Del Corral, Gabriel; Forte, Antonio J.; Ciudad, Pedro; Kim, Esther A.; Langstein, Howard N.; Manrique, Oscar J. (2021). "Regret after Gender-affirmation Surgery: A Systematic Review and Meta-analysis of Prevalence". Plastic and Reconstructive Surgery – Global Open (kwa en-US) 9 (3): e3477. doi:10.1097/GOX.0000000000003477. 
 10. 10.0 10.1 James, Sandy E.; Herman, Jody L.; Rankin, Susan; Keisling, Mara; Mottet, Lisa; Anafi, Ma'ayan (2016). "De-Transitioning". The Report of the 2015 U.S. Transgender Survey (Ripoti). Washington, DC: National Center for Transgender Equality. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo January 21, 2018. Iliwekwa mnamo March 18, 2019.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
 11. 11.0 11.1 Turban, J.L.; Loo, S.S.; Almazan, A.N.; Keuroghlian, A.S. (May 2021). "Factors Leading to "Detransition" Among Transgender and Gender Diverse People in the United States: A Mixed-Methods Analysis". LGBT Health. doi:10.1089/lgbt.2020.0437.  Check date values in: |date= (help)
 12. Doyle, David Matthew; Lewis, Tom O. G.; Barreto, Manuela (2023). "A systematic review of psychosocial functioning changes after gender-affirming hormone therapy among transgender people". Nature Human Behaviour (kwa Kiingereza) 7 (8): 1320–1331. ISSN 2397-3374. doi:10.1038/s41562-023-01605-w. 
 13. "Hormone Therapy for Gender Dysphoria May Raise Cardiovascular Risks". American College of Cardiology. Iliwekwa mnamo 2024-04-09. 

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbadili jinsia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.