Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Mbadili jinsia

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makakala haina vyanzo. Hata nukuu kwenye tanbihi haionyeshi chazo chake. Kipala (majadiliano) 06:41, 24 Machi 2021 (UTC)[jibu]

Nina maulizo kidogo, Je tunahada ya kuwa n makala hii? ... Olimasy (majadiliano)

Samahani, sijaelewa swali lako. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:58, 16 Septemba 2022 (UTC)[jibu]
Samahani nilikosea kuandika. nilikua na maana ya kwamba, Tunahaja kwenye jamii yetu kuwa na makala juu ya mada hii?. -- Olimasy (majadiliano)
Nadhani haja lipo, maana watu ambao jinsia ya kimwili na jinsia ya nafsi ni tofauti wako kila nchi, kama jamii inakubali au la. Ila naona a) lemma ya Kiswahili haifai. Kila kamusi ninaloangalia ina maana ya "mwanaume anayefanya ngono na mwanaume mwingine", ambayo si maana ya transgender. b) sijasoma makala ila kwenye mistari za kwanza napata maswali kidogo. Sina muda zaidi sasa lakini kazi ipo. Kipala (majadiliano) 13:53, 16 Septemba 2022 (UTC)[jibu]
Jina la makala nimeliacha kama nilivyolikuta kwa kuwa sijaona lingine la kufaa. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:39, 17 Septemba 2022 (UTC)[jibu]
Vipi tukiandika ushoga? haviendani? na kama maana moja na ushoga tunafanyeje, makala iachwe au ifutwe? -- Olimasy (majadiliano)
Makala haiishii katika ushoga wa kawaida. Ni hatua ya mbele zaidi. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:35, 17 Septemba 2022 (UTC)[jibu]
Sawa nimekuelewaǃ Tukaribishe na wengine waweze kuchangia juu ya maada hii kuhusu ushoga na usenge tuone kama tunaweza kuwa nazo, kwasababu tulisha wahi kujadiri kuhusu maadili yetu na maoni ya Wikimedia foundation kuhusu tamaduni na utaratibu wa makundi mbalimbali. Au wewe waonaje? Olimasy (majadiliano) 15:37, 17 Septemba 2022 (UTC)[jibu]
Ndugu, suala la maadili yetu lipo kweli, lakini hatuwezi kujifanya hatujui kinachotokea sehemu nyingine ya dunia hii, kama alivyoandika Kipala hapo juu. Ni kuona namna ya kuzungumzia jambo ili kujenga na si kubomoa kwa kufuata kasumba! Suala la jina la Kiswahili lizidi kujadiliwa. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 05:43, 18 Septemba 2022 (UTC)[jibu]