Nenda kwa yaliyomo

Moshi (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Moshi
Jiji la Moshi is located in Tanzania
Jiji la Moshi
Jiji la Moshi

Mahali pa mji wa Moshi katika Tanzania

Majiranukta: 3°20′24″S 37°20′24″E / 3.34000°S 37.34000°E / -3.34000; 37.34000
Nchi Tanzania
Mkoa Kilimanjaro
Wilaya Moshi Mjini
Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi mjini
Msikiti Mkuu wa Moshi

Moshi ni makao makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.

Wakazi

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002, mji huu una wakazi wapatao 144,739 [1]. Kabila linaloongoza kwa idadi ya wakazi wa mji wa Moshi ni Wachagga. Kuna makabila mengi kama Wapare, Wanyakyusa, Wasukuma, Warangi, Wasambaa n.k. Wachagga wanapenda vyakula vinavyopikwa kwa kutumia ndizi kama vile mtori, kitawa, na machalari.

Wakazi wengi wa Moshi ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara. Watu wengi wanaenda Moshi kufanya kazi na kurudi nyumbani jioni.

Ukuaji wa mji wa Moshi hauendani na mipango halisi ya 'Mipango Miji'. Hii inatokana na kutokufuatiliwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu uendelezaji wa miji.

Hali ya Hewa

Moshi ni mji wenye baridi katika miezi ya Juni mpaka Agosti na kipindi cha joto katika miezi ya Oktoba hadi katikati ya Januari.

Utalii

Mji wa Moshi una mandhari nzuri ya kuvutia watalii. Watalii hupenda sana mji wa Moshi kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na huduma muhimu kama mahoteli na usafiri.

Elimu

Mji wa Moshi una vyuo vikuu vitatu:

Utawala

Kiutawala mji wa Moshi ni wilaya ya Mkoa wa Kilimanjaro. Ndani yake kuna kata 15 ambazo ni Bondeni, Kaloleni, Karanga, Kiboroloni, Kiusa, Korongoni, Longuo, Majengo, Mawenzi, Mji Mpya, Msaranga, Njoro, Pasua, Rau na Kilimanjaro.

Marejeo

  1. 2002 Population and Housing Census General Report, Government of Tanzania. Ilitazamiwa 17-01-2008(Kiingereza)
Kata za Wilaya ya Moshi Mjini - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania

Bomambuzi | Bondeni | Kaloleni | Karanga | Kiborloni | Kilimanjaro | Kiusa | Korongoni | Longuo B | Majengo | Mawenzi | Mfumuni | Miembeni | Mji Mpya | Msaranga | Ng'ambo | Njoro | Pasua | Rau | Shirimatunda | Soweto


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Moshi (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.