Nenda kwa yaliyomo

Mohenjo-Daro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mohenjo Daro)
Ramani ya miji mikubwa zaidi ya utamaduni wa Harappa.
Sanamu ya "Binti anayecheza" iliyopatikana Mohenjo-Daro.
Sanamu ya kiongozi anayeaminiwa kuwa mfalme na kuhani mnamo 2,500-1,500 BK iliyopatikana kati ya maghofu ya Mohenjo-Daro.

Mohenjo-Daro [1] ilikuwa mji mkubwa katika ustaarabu wa Indus uliostawi kwenye bonde la Mto Indus. Iko katika jimbo la Sindh, Pakistan ya leo.

Mji ulijengwa mnamo mwaka 2600 KK na kuwa kati ya miji ya kwanza duniani inayojulikana. Mohenjo-Daro ilistawi wakati mmoja na tamaduni za Misri ya Kale na Mesopotamia.

Mabaki ya mji yamepokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mohenjo-Daro ilijengwa mnamo karne ya 25 KK.[2] Ilikuwa kati ya miji mikubwa ya utamaduni wa Harappa ulioenea katika bonde la mto Indus. [3] Utamaduni huo ulianza mnamo mwaka 3000 KK na kuenea juu ya sehemu kubwa za Pakistan na Uhindi ya Kaskazini ya leo. Miji muhimu iliyotambuliwa na wanaakiolojia ilikuwa Harappa, Mohenjo-Daro, Lothal, Kalibangan, Dholavira na Rakhigarhi.

Mohenjo-Daro ilikuwa mji mkubwa wa Zama za Shaba yaani kipindi ambapo watu walikuwa wameshaanza kutumia metali badala ya zana za mawe tu lakini bado hawakutumia chuma.

Wataalamu wametambua kiwango cha juu wa kupangwa kwa mji huu. Wajenzi wake walitumia tayari matofali yaliyosanifishwa kwa kutumia vipimo vya sentimita 6 × 13 × 27.

Mji wote ulikuwa na mfumo wa visima vya maji zaidi ya 700 na pia mifereji kwa maji machafu. Watu wake walikuwa pia na mwandiko ambao haujatafsiriwa. [4]

Mnamo mwaka 1900 KK utamaduni wa Harappa uliporomoka kwa sababu ambazo hazikueleweka bado na wakazi waliondoka mjini.[2][5]

Maghofu ya majengo ya Mohenjo-Daro.
  1. (kwa Kiurdu: موئن جودڑو kwa maana ya "kilima cha wafu")
  2. 2.0 2.1 Ancientindia.co.uk. Retrieved 2012-05-02.
  3. Beck, Roger B. et al 1999. World History: patterns of interaction. Evanston, IL: McDougal Littell. ISBN 0-395-87274-X.{{cite book}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link)
  4. Dani A.H. 1992. Critical assessment of recent evidence on Mohenjo-daro. Second International Symposium on Mohenjo-daro, 24–27 February 1992.
  5. Kenoyer, Jonathan Mark 1998. Indus cities, towns and villages. Ancient Cities of the Indus Valley Civilization. Islamabad: American Institute of Pakistan Studies. p.65
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mohenjo-Daro kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.