Nenda kwa yaliyomo

Namba sanifu ya kimataifa ya vitabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka ISBN (identifier))
Namba sanifu ya kimataifa ya vitabu (ISBN) kwa mwandiko wa tarakimu na msimbo pau

Namba sanifu ya kimataifa ya vitabu (en:International Standard Book Number) inayojulikana kwa kifupi chake cha ISBN ni namba ya kipekee ya utambulisho wa vitabu viuzwavyo kibiashara. Inasaidia kujua kwa uhakika ni kitabu kipi kinachoagizwa na mteja na kutumwa kutoka wachapishaji kwenda dukani.

ISBN inapangwa kwa kila toleo na tofautisho (isipokuwa marekebisho) la kitabu. Kwa mfano, Kitabu cha kielektroniki, paperback na toleo gumu (hardcover) la kitabu kilekile kila moja itakuwa na ISBN tofauti. ISBN ina urefu wa tarakimu 13 kama iliwekwa kuanzia tarehe 1 Januari 2007, na urefu wa tarakimu 10 kama iliwekwa kabla ya mwaka 2007.

Namna ya kuweka ya ISBN inategemea taifa lenyewe na hutofautiana kutoka nchi hadi nchi, mara nyingi inategemea na ukubwa wa sekta ya uchapishaji ndani ya nchi. Kila namba inaweza kuonyeshwa kwa tarakimu au msimbo pau.