Mkutano wa Kijiografia wa Brussels

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mkutano wa Kijiografia wa Brussels (kwa Kiingereza: Brussels Geographic Conference) ulifanyika Brussels, Ubelgiji mnamo Septemba 1876. Mkutano uliitishwa na Mfalme Leopold II wa Ubelgiji. Katika mkutano huo alialika wataalamu mashuhuri karibu arobaini, haswa mabingwa katika jiografia, pamoja na watu tajiri waliojulikana kama wafadhili.

Kabla ya wageni kurudi katika nchi zao, waliamua kuanzisha Ushirika wa Kimataifa wa Afrika (International African Association). Mpango huo mwishowe ulifungua njia kwa kuundwa kwa Dola Huru la Kongo, lililokuwa koloni la binafsi la mfalme.

Hali halisi nia ya Leopold katika kuitisha mkutano ilihusiana na mipango yake ya kuanzisha koloni na kushindwa kwa mipango yake ya kupata Ufilipino kutoka Hispania. Alianza kuangalia Afrika baada ya kusoma taarifa ya mpelelezi Verney Lovett Cameron aliyewahi kuvuka Afrika kutoka Bahari ya Hindi hadi Atlantiki katika miaka 1873 - 1875 na kuandika kwamba kitovu cha Afrika "ni nchi yenye utajiri kupita kiasi wa dhahabu, shaba, fedha na makaa mawe inayosuburi kuendelezwa".

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

  • Émile Banning, Africa and the Brussels geographical conference, translated by Richard Henry Major, London : Sampson Low, Marston, Searle & Rivington, 1877
  • Fondation du Congo, Memoires de Emile Banning, 1927