Mkunde Chachage

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkunde Chachage

Amezaliwa Juni 2 1984
Dar es Salaam
Nchi Tanzania
Kazi yake Mhadhiri na mtafiti wa kinga mwili
Cheo Mwana sayansi


Mkunde Chachage (alizaliwa Juni 2, 1984) ni mhadhiri na mtafiti wa kinga-mwili katika Chuo Shirikishi cha Afya na Sayansi za Afya cha Mbeya kilichopo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM - MCHAS). [1] Chachage pia ni mtafiti katika Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba katika kituo cha utafiti wa afya cha Mbeya (NIMR - MMRC). [2] Utafiti wake umejikita kwenye kinga mwili na magonjwa ya kuambukiza ya binadamu hasa Kifua Kikuu (TB), VVU na maambukizi ya minyoo. [3]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Chachage anatoka kwenye familia ya wanataaluma mashuhuri na wanaharakati. Alizaliwa Dar es Salaam na marehemu Profesa Chachage Seithy Loth Chachage na Demere Kitunga akiwa mmoja wa watoto wa nne. Baba yake alikuwa msomi mashuhuri, mchambuzi wa kisiasa na mwandishi. Mama yake ni mwanaharakati wa usawa wa kijinsia na mwandishi mashuhuri [4] [5], mhariri na mchapishaji nchini Tanzania. [6] [7] Ndugu zake wawili pia ni wanataaluma, wakiwemo Chambi Chachage , ambaye ni mwanataaluma wa taaluma za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Princeton na mchambuzi wa kisiasa, [8] pamoja na Rehema Chachage, ambaye ni mwanataaluma katika Chuo Kikuu cha Vienna, Austria, [9] na mwanasanaa. [10]

Chachage amekulia jijini Dar es Salaam, Tanzania, ambapo alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Mlimani na shule ya msingi Dar es Salaam Independent, kabla ya kumaliza masomo ya sekondari katika shule ya sekondari ya Aga Khan Mzizima. Hivi sasa ameolewa na Keremba Brian Warioba, ambaye alishirikiana naye kuanzisha kampuni ya biashara ya kijamii (social entreprise)'na kupata mtoto mmoja.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Chachage ana shahada ya uzamili (PhD) ya afya ya Kimataifa kwenye kinga ya mwili kutoka Chuo Kikuu cha Ludwig Maximilian cha Munich, Ujerumani, aliyoipata mnamo mwaka 2013. Andiko lake la shahada ya uzamili lilichunguza mabadiliko ya mfumo wa kinga ya binadamu yanayosababishwa na maambukizi ya minyoo na athari zake kupata maambukizo ya VVU au kuzorota kwa afya za watu wanaoishi na VVU [11] Alipata Shahada ya sayansi katika Baiolojia ya Molekula na Celi kutoka Chuo Kikuu cha Capetown mnamo 2007, ikifuatiwa na digrii ya honors mwaka uliofuata kutoka taasisi hiyo hiyo. 

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Chachage alijiunga na Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba kituo ca utafiti wa afya cha Mbeya (NIMR-MMRC) mnamo mwaka 2009 kama mtafiti. [12] Alirudi katika kituo hicho cha utafiti mara tu baada ya kupata shahada ya uzamili, ambapo alipewa nafasi ya kuongoza maabara ya utafiti wa kinga mwili ikitilia mkazo kwenye utafiti unaohusiana na vitambuzi vya magonjwa kwenye magonjwa ya TB, VVU na VVU-HPV. [3]

Chachage ni mshirika wa African Academy of Science katika kundi la tatu kati ya miaka 2018 - 2022. [12] Pia amekua mshirika wa masomo baada ya shahada ya uzamili katika Taasisi ya Burnet, Melbourne, Australia, kati ya miaka 2015 - 2016 [3] na ushirika wa Afrika - Oxford (AfOx) kwa watafiti wa Kiafrika mnamo 2020, ambayo inamruhusu kushirikiana na watafiti Chuo Kikuu cha Oxford katika utafiti unaoendelea wa vijidudu. [13] Chachage pia ni mshiriki wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ukimwi (IAS) ambapo anashiikiana na wanasayansi wengine kwenye utafiti na teknolojia mpya za tiba ya VVU. [14] [15]

Mbali na kazi ya utafiti, amefundisha kozi juu ya kingamwili ya magonjwa ya kuambukiza katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika ya Nelson Mandela (NM-AIST), huko Arusha, Tanzania . [3] Mnamo Januari 2019 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama mhadhiri na mtafiti akifundisha na kufanya utafiti juu ya masomo yanayohusiana na kingamwili ya binadamu. [1]

Chachage pia ni mjasiriamali ambaye alianzisha kampuni ya kijamii ambayo inasaidia wakulima wadogo wa kahawa wa Tanzania kupata soko la mavuno yao. [16]

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

  • Mwanasayansi bora wa Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba (NIMR) iliyoyolewa na Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba (NIMR) (2018) [16]
  • Mtafiti bora wa kisayanis wa Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba (NIMR) - Kituo cha utafiti cha Mbeya aliyopewa na Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba (NIMR) kwa kutambua kazi zake za utafiti kwenye vimelea vya VVU na TB (2018)
  • Tuzo ya Mwanasayansi Bora wa Kike ya Dkt. Maria Kamm aliyopewa na Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Tiba (NIMR) (2012) [17]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Mkunde Chachage". University of Dar es Salaam. 
  2. "Mkunde Chachage". FAIS Legacy Project. 
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 "Dr. Mkunde Chachage". TBSequel. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-01. Iliwekwa mnamo 2021-04-15. 
  4. "Demere Kitunga African Feminist". African Feminist Forum. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-15. Iliwekwa mnamo 2021-04-15. 
  5. "Leading Feminist and Literacy advocate". The Citizen Newspaper. 
  6. "Demere Kitunga". Barranca Press. 
  7. "Feminism column". Daily News, the National Newspaper. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-14. Iliwekwa mnamo 2021-04-15. 
  8. "Africa: Rethinking in action!". Society for International Development. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-15. Iliwekwa mnamo 2021-04-15. 
  9. "Staff list University of Viana Department of theatre, film and media studies". University of Vienna. 
  10. "Rehema Chachage: The intimacy and harshness of African women’s rituals". Urban Africans. 
  11. "CIH - LMU alumna". Ludwig Maximilian University of Munich. 
  12. 12.0 12.1 "Chachage Mkunde | The AAS". www.aasciences.africa. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-09-21. Iliwekwa mnamo 2021-04-15. 
  13. "AfOx Fellows 2020". Africa-Oxford fellowship. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-11. Iliwekwa mnamo 2021-04-15. 
  14. "AIS fellow Mkunde Chachage". International AIDS Society. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-11. Iliwekwa mnamo 2021-04-15. 
  15. "AIS global fellows". International AIDS Society. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-12. Iliwekwa mnamo 2021-04-15. 
  16. 16.0 16.1 "Communal shamba". Five Senses. "Communal shamba". Five Senses.
  17. "Dr. Maria Kamm Best Woman Scientist Award". UDADISI. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-12. Iliwekwa mnamo 2021-04-15. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkunde Chachage kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.