Nenda kwa yaliyomo

Mitalojia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makala hii kuhusu "Mitalojia" inatumia neno au maneno ambayo si ya kawaida; matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Mitalojia (kutoka Kiingereza metrology) ni elimu ya upimaji[1]. Inalenga kuweka msingi kwa maelewano kuhusu vizio na matumizi yake ambayo ni jambo la msingi kwa shughuli za kimataifa.

Neno limeundwa na "mita" (kipimo cha kimataifa cha umbali; kiasili Kigiriki μετρον) na "lojia", ambayo ni kiambishi kinachotaja sayansi au elimu ya jambo fulani[2]

Asili ya sayansi ya upimaji ya kisasa ilipatikana wakati wa mapinduzi ya Kifaransa. Wakati ule wingi wa vizio vya urefu vilivyokuwa kawaida, mara nyingi kwa kutumia vizio vya kimwili[3], wataalamu walipendekeza kutumia kizio kilichorejelea chanzo cha kimazingira yaani sehemu ya mzingo wa Dunia. Hii iliunda mfumo wa vizio vilivyokadiriwa kidesimali mnamo mwaka 1795. Mfumo huo ulianza kutumiwa pia na nchi nyingine na hatimaye kuleta mfumo wa vipimo sanifu vya kimataifa[4].

Matawi ya mitalojia

[hariri | hariri chanzo]

Wataalamu wa mitalojia huangalia hasa mambo matatu:[5][6]

1. Ufafanuzi wa vizio vya upimaji. Huu unahusu hasa kurejelea vizio vya upimaji kwa vizio vya kifizikia, tofauti na vizio vya kimazingira kama awali. Mfano mita ilifafanuliwa kiasili kama sehemu moja ya milioni ya umbali kutoka ncha ya kaskazini hadi ikweta. Baadaye imetambulikana kwamba umbo la Dunia si tufe kamili, umbali kati ya ncha hiyo na ikweta ni tofauti kutegemeana na sehemu unapopimwa. Hivyo umbo la Dunia halifai tena kwa ufafanuzi wa kizio sahihi. Wataalamu walitafuta ufafanuzi wa kifizikia ambao hautegemei vizio vinavyoweza kubadilika. Mwaka 1983 Kongamano la 15 la Uzani na Vipimo (General Conference on Weights and Measures; kifupi: CGPM) uliamua kufafanua mita kulingana na kasi ya nuru ikiwa sawa na umbali unaopitiwa na nuru katika sehemu ya 1/299 792 458 ya sekunde moja[7].

2. Kuhakikisha na kutathmini matumizi ya vizio hivi katika tasnia na biashara

3. Matumizi ya vizio vya upimaji katika sheria za nchi na za kimataifa.

  1. "What is metrology? Celebration of the signing of the Metre Convention, World Metrology Day 2004". BIPM. 2004. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-27. Iliwekwa mnamo 2018-02-21.
  2. Kamusi ya KAST ilipendekeza istilahi "metalojia"; katika wikipedia hii tunatumia tahajia "mita", si meta; pia tunaona ugumu wa kufanana mno na istilahi ya Kiswahili kwa "metallurgy" (sayansi ya metali na aloi zao). Kwa namna nyingine umbo la Kiswahili lingekuwa pia "metrolojia", lakini hii imetumiwa tayari kama tahajia badala mojawapo ya elimu ya hali ya hewa (metorolojia). Tunakaribisha maoni kama tuache neno la kigeni na kubaki tu na "elimu upimaji"
  3. Kama vile futi, shibiri, wanda, ambavyo viko tofauti baina mtu na mtu, na vilisaninifishwa kieneo tu, kwa hiyo ilikuwa kawaida kukuta vizio tofauti kila mahali.
  4. "Resolution 12 of the 11th CGPM (1960)". Bureau International des Poids et Mesures. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Mei 2013. Iliwekwa mnamo 28 Februari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Czichos, Horst; Smith, Leslie, whr. (2011). Springer Handbook of Metrology and Testing (tol. la 2nd). 1.2.2 Categories of Metrology. ISBN 978-3-642-16640-2. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-07-01.
  6. Collège français de métrologie [French College of Metrology] (2006). Placko, Dominique (mhr.). Metrology in Industry – The Key for Quality (PDF). ISTE. 2.4.1 Scope of legal metrology. ISBN 978-1-905209-51-4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 2012-10-23. ... any application of metrology may fall under the scope of legal metrology if regulations are applicable to all measuring methods and instruments, and in particular if quality control is supervised by the state.
  7. Definition of the metre Archived 27 Mei 2020 at the Wayback Machine., Resolution 1 of the 17th CGPM (1983)]
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mitalojia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.