Shibiri
Mandhari
Kwa mmea mwenye jina la karibu angalia hapa Mshubiri
Shibiri (kawaida zaidi: shubiri kutoka Kiarabu شبر, shibr; pia: futuri) ni kipimo cha urefu wa takriban cm 20 - 25.
Ni kati ya vipimo asilia vya Kiswahili, ni umbali mkubwa kati ya kidole gumba na kidole cha mwisho kwenye mkono mmoja.
Inafanana na morta, lakini ni ndefu zaidi. Shubiri ni takriban nusu ziraa.
Shibiri si kipimo sanifu, lakini katika maisha ya kila siku inasaidia sana. Mtu akijua urefu wa shibiri yake anaweza kupima vitu vingi haraka. Kwa sababu mtu hutembea na mkono wake kila saa, tofauti na futi au chenezo. Hivyo kuna ushauri wa kwamba kila mtu apime shibiri yake na kuikumbuka kwani itamsaidia kila mahali.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- makala "Shubiri, shibiri" katika kamusi ya Velten