Nenda kwa yaliyomo

Dhiraa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ziraa)
Ziraa

Dhiraa (pia ziraa[1], kutoka Kiarabu ذراع dhiraac; ing. ni cubit au ell) ni kipimo cha kihistoria cha urefu cha takriban sentimita 50. Iliitwa pia "mkono".

Ni kati ya vipimo asilia vya Kiswahili, ni umbali mkubwa kati ya kidole kikubwa na kisugudi au kiko cha mkono wake.

Dhiraa inalingana na kipimo cha shibiri; dhiraa moja ni sawa na shibiri mbili.

Kipimo cha kale sana

[hariri | hariri chanzo]

Dhiraa iko kati ya vipimo vya kale kabisa duniani. Inatajwa katika Biblia, kwa mfano Mwa. 6,15-16; Mwa. 7,20; Kut. 25,10.17.23; 1 Fal. 7 na penginepo. Pamoja na dhiraa ya kawaida kulikuwa pia na dhiraa ya pekee yenye urefu kidogo zaidi inayotajwa katika Kitabu cha Ezekieli 40,5 na Ez. 43,13.

Katika milki ya Misri ya Kale dhiraa iliwahi kusanifishwa mapema. Mafimbo yanayoonyesha alama za dhiraa zilipatikana katika makaburi ya Misri yaliyofungwa mnamo mwaka 1300 KK.[2] Dhiraa hii ilikuwa dhiraa ndefu na mafibo yalionyesha kipimo cha milimita 523.5 hadi 529.2 [3] ikiaminiwa kuna uwezekano kuwa sawa na dhiraa ndefu inayotajwa katika Kitabu cha Ezekieli[4].

  1. Krapf katika kamusi yake (mwaka 1882) anaandika "thiraa".
  2. Arnold Dieter (1991). Building in Egypt: pharaonic stone masonry. Oxford: Oxford University Press. ISBN 978-0-19-506350-9. p.251.
  3. Richard Lepsius (1865). Die altaegyptische Elle und ihre Eintheilung (in German). Berlin: Dümmler. p. 14–18
  4. Makala kuhusu vipimo "Maße und Gewichte" katika tovuti ya bibelwissenschaft.de (tovuti ya "Elimu ya Biblia" ya Shirika la Biblia Ujerumani), iliangaliwa Machi 2017