Nenda kwa yaliyomo

Misaada ya kimataifa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Misaada ya kimataifa ni neno linalotumiwa katika jumuiya ya mandeleo ya kimataifa kuhusu pesa inayotolewa na nchi tajiri kwa nchi maskini. Misaada ya kimataifa inaweza kutolewa na nchi binafsi au na mashirika ya nchi nyingi, kama Benki ya Dunia au Umoja wa Mataifa (UN). Misaada ya kimataifa ina lengo la kupunguza umasikini kote duniani, ni njia ya nchi za wafadhili kupata ushawishi pia wa kisiasa.

Nchi zinaweza kutoa misaada kwa nchi zingine kwa ajili nyingi, kama kwa kijeshi au mandeleo. Makala hii ni kuhusu misaada ya kimataifa ya mandeleo tu. Misaada ya kimafaita inaweza kwenda serikali za nchi za wapokeaji, au mashirika ya NGO kufanya programu maalum. Misaada ya mandeleo inaweza kutolewa kwa ajili nyingi, kama mandeleo ya uchumi, elimu, afya, au mandeleo ya mashirika ya serikali katika nchi za wapokeaji.

Mashirika na nchi kuu za wafadhili

[hariri | hariri chanzo]

Sekta ya misaada kimataifa ni kubwa sana. Kuna mashirika tofauti nyingi na nchi nyingi zinazotoa misaada na kufanya programu ya mandeleo. Mashirika na nchi hizi zinaitwa wafadhili. Sehemu hii itaelezea kidogo kuhusu mashirika na nchi kuu za wafadhili.

Mashirika ya Wafadhili

[hariri | hariri chanzo]

Moja wa mashirika makubwa katika misaada ya kimataifa ni Benki ya Dunia. Benki ya Dunia inajumuisha ya nchi nyingi. Nchi za wanachama zinachangia pesa na Benki ya Dunia inatumia pesa hii kutoa mikopo na kufanya programu katika nchi maskini, kama programu kwa maji safi, elimu, au afya.[1]

Mpango wa Mandeleo wa Umoja wa Mataifa

Shirika lingine ambalo ni sawa na Benki ya Dunia ni Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF). Shirika hili linajumuisha ya nchi nyingi pia, na linatoa mikopo kwa nchi zinazohitaji msaada. Hata hivyo, IMF ni tofauti na Benki ya Dunia kwa sababu ina malengo ya utulivu wa kifedha na biashara ya kimataifa.[2]

Mpango wa Mandeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) ni shirika lingine la misaada ya kimataifa. UNDP ni sehemu ya Umoja wa Mataifa, na ni sawa na Benki ya Dunia. Inalenga kupunguza umasikini kote duniani na iliumba malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).[3] SDGs ni muhimu sana katika jumuiya ya mandeleo ya kimataifa.

Pia, kuna mashirika ya misaada ya kimataifa kwa mabara maalum. Kwa mfano, Benki ya Mandeleo ya Afrika (AfDB) na Benki ya Mandeleo ya Asia (ADB) yanajumuisha ya nchi za kote duniani, lakini yana malengo ya mandeleo katika Afrika au Asia tu.

Nchi za Wafadhili

[hariri | hariri chanzo]

Jumuiya kuu ya nchi za wafadhili inaitwa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD). Nchi za OECD zinajumuisha Marekani, Kanada, nchi nyingi za Ulaya ya Magharibi, Korea Kusini, Israel, Uturuki, na nchi nyingine. OECD lina nchi za wanachama thelathini na sita.[4] Nchi za OECD ni, kwa msingi, nchi tajiri sana za dunia. Nchi hizi ni nchi za wafadhili wa jadi. Zinatoa misaada ya kimataifa ya ubinafsi, lakini zote ni katika Kamati ya Usaidizi wa Maendeleo (DAC) ya OECD. Mwaka 2017, DAC ilitoa bilioni $99.5 kwa nchi zinazoendelea.[4]

Nchi ya wafadhili kubwa nyingine ni China. China ni mpya kwa jumuiya ya misaada ya kimataifa na si nchi ya wanachama ya OECD. Hata hivyo, China inakuwa muhimu sana kama uchaguzi badili kwa wafadhili wa Magharibi, hasa katika nchi za Afrika na Amerika ya Kusini. Watu wengine wanasema kwamba misaada ya kimataifa kutoka China ni tofauti kidogo kwa sababu China inatumia misaada kama njia kukua uchumi wake.

Misaada ya kimataifa katika Afrika Mashariki

[hariri | hariri chanzo]

Nchi za Afrika Mashariki zimepata misaada ya kimataifa mengi, hasa kutoka Marekani na China. Sehemu hii itaelezea kuhusu misaada ya kimataifa katika Afrika Mashariki, ikiwamo idadi ya misaada na matumizi ya misaada katika nchi hizi.

Uchumi wa Burundi inategemea na misaada ya kimataifa sana. Mwaka 2016, Burundi ilipokea milioni $737 ya misaada ya kimataifa kwa ujumla.[5] Takriban yote ya misaada katika Burundi inatumiwa katika sekta ya afya.[6]

Nchi za Afrika Mashariki

Nchi ya Kenya ilipokea bilioni $2.2 ya misaada ya kimataifa mwaka 2016.[5] Kama nchi nyingine nyingi katika Afrika, misaada mengi inatumiwa kwa programu za afya. Misaada mengi katika Kenya inatumiwa kwa mandeleo ya uchumi pia. China inatoa misaada mengi kwa nchi ya Kenya, hasa kwa ajili ya miradi ya ujenzi na usafiri.[6]

Rwanda imepokea misaada mengi tangu ya uangamizaji wa kabila mwaka 1994. Rwanda ilipokea bilioni $1.2 ya misaada mwaka 2016.[5] Misaada mengi katika Rwanda inatumiwa kwa programu za afya na kurekebisha ya usalama.[6]

Tanzania

[hariri | hariri chanzo]

Tanzania ni nchi mpokeaji kubwa ya misaada ya kimataifa ya Afrika Mashariki. Mwaka 2016, Tanzania ilipokea bilioni $2.3 ya misaada ya kimataifa kutoka mashirika na nchi tofauti.[5] Misaada mengi inatumiwa kwa programu za afya.[6] Pia, China inatoa misaada mengi kwa Tanzania na imefanya miradi mikubwa katika Tanzania kama reli ya TAZARA.[7]

Mwaka 2016, nchi ya Uganda ilipokea bilioni $1.8 ya misaada ya kimataifa.[5] Misaada kwa Uganda inatumiwa zaidi kwa programu za afya na mandeleo ya uchumi. Uganda imepokea misaada ya ubinadamu kwa wakimbizi pia.[6]

  1. "World Bank Group - International Development, Poverty, & Sustainability". World Bank (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-03-04.
  2. "IMF -- International Monetary Fund Home Page". www.imf.org. Iliwekwa mnamo 2019-03-04.
  3. "UNDP - United Nations Development Programme". UNDP (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-03-06. Iliwekwa mnamo 2019-03-04.
  4. 4.0 4.1 "ODA Official development assistance: disbursements". www.oecd-ilibrary.org. Iliwekwa mnamo 2019-03-04.
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 Development at a Glance: Statistics by Region. 2. Africa. 2018http://www.oecd.org/dac/financing-sustainable-development/development-finance-data/Africa-Development-Aid-at-a-Glance-2018.pdf
  6. 6.0 6.1 6.2 6.3 6.4 "ForeignAssistance.gov". www.foreignassistance.gov. Iliwekwa mnamo 2019-03-04.
  7. "TAZARA | Tanzania-Zambia Railway Authority". www.tazarasite.com. Iliwekwa mnamo 2019-03-04.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Misaada ya kimataifa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.