Milima ya kuvukia Antaktiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Antaktiki (mstari kahawia: Milima ya kuvukia Antaktiki).

Milima ya kuvukia Antaktiki (kwa Kiingereza: Transantarctic Mountains) ni safu ya milima katika bara la Antaktiki. Inagawa bara hilo kuwa sehemu mbili za mashariki na magharibi. Inaenea kwa zaidi ya km 3,200.

Miinuko ya juu ni zaidi ya mita 4,500 juu ya usawa wa bahari, mrefu zaidi ni Mlima Kirkpatrick (m 4528) katika Nchi ya Viktoria karibu na Bahari ya Ross. Miinuko ya juu zaidi zinaonekana juu ya ganda la barafu linalofunika bara lote lenye unene wa mita 3,000 lakini sehemu duni zaidi ya milima ziko chini ya uso wa barafu.

Rasi ya Antaktiki upande wa magharibi si sehemu ya milima hiyo.

Kutokana na baridi kali ya mazingira hakuna wanyama wala mimea: uhai pekee ni viumbehai sahili kama vile bakteria, [1] mwani na kuvu.

Jina la "Transantarctic Mountains" ilitumiwa kwanza mnamo 1960, kwenye makala ya mtaalamu wa jiolojia Warren Hamilton. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sokol, Eric; Craig W. Herbold; Charles K. Lee; S. Craig Cary; J. E. Barrett (Nov 2013). "Local and regional influences over soil microbial metacommunities in the Transantarctic Mountains". Ecosphere 4: art136. doi:10.1890/es13-00136.1. Iliwekwa mnamo 8 January 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Hamilton, Warren B. (1960). "New interpretation of Antarctic tectonics." Geological Survey Research 1960 — Short Papers in the Geological Sciences, pp. B379–380. Washington DC: US Geological Survey.