Miguel de Cervantes

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Cervantes alivyochorwa.

Miguel de Cervantes Saavedra (29 Septemba 154723 Aprili 1616) alikuwa mwandishi wa Hispania anayesifiwa kama mwandishi bora kabisa wa nchi yake. Mara nyingi riwaya yake Don Quishote inahesabiwa kati ya vitabu muhimu zaidi vya fasihi ya Ulaya nzima.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Cervantes alizaliwa kama mtoto wa nne kati ya saba wa mganga. Hakuna habari kamili juu ya maisha yake kama kijana.

Alipokuwa na miaka 23 alijiunga na jeshi la wanamaji wa Hispania akashiriki kwenye mapigano ya Lepanto dhidi ya milki ya Osmani alipojeruhiwa na kupotewa na mkono wa kulia.

Mwaka 1575 alikamatwa na maharamia Waalgeria akawa mfungwa hadi kununuliwa na wamonaki Wakristo waliomrudisha nyumbani.

Tangu mwaka 1584 alianza kuandika lakini mwanzoni bila mafanikio ya kipesa. Alipata kazi kama mkusanyaji kodi lakini alishindwa kuonyesha hesabu safi ya mikusanyo yake akatupwa jela. Hapo alianza kazi ya kuandika riwaya yake ya "El ingenioso Hidalgo Don Quijote de la Mancha" iliyotolewa mwaka 1605 na sehemu ya pili ikafuata mwaka 1615. Kitabu hiki kilipendwa na kutafsiriwa katika lugha mbalimbali za Ulaya.

Hata hivyo alikufa maskini na sifa zake zilikua baada ya kifo chake tu.

Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki, tena mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.

Inkwell icon - Noun Project 2512.svg Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Miguel de Cervantes kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.