Nenda kwa yaliyomo

Mmepulu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Micropotamogale)
Mmepulu
Mmepulu mkubwa kwenye Makumbusho ya Historia ya Asili, London (Potamogale velox)
Mmepulu mkubwa kwenye Makumbusho ya Historia ya Asili, London
(Potamogale velox)
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda ya juu: Afrotheria (Wanyama wenye asili ya Afrika)
Oda: Afrosoricida (Wanyama kama tandaraka)
Nusuoda: Tenrecomorpha (Wanyama kama tandaraka)
Familia: Potamogalidae (Wanyama walio na mnasaba na wamepulu)
Allman, 1865
Ngazi za chini

Jenasi 2, spishi 3:

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wamepulu (kutoka Kiasoa: amepulu) au katewe (kutoka Kiluvale: katewe) ni wanyama wadogo wa familia Potamogalidae. Hawa ni wanyama wa maji ambao wanatokea misitu ya mvua ya Afrika kusini kwa Sahara. Wanafanana na fisi-maji wadogo lakini hawana mnasaba na hawa. Wana mnasaba na tandaraka wa Madagaska. Wale wa jenasi Micropotamogale wana mwili wa sm 12–20 na mkia wa sm 10–15; wale wa Potamogale wana mwili wa sm 30–35 na mkia wa sm 25–29. Spishi zote zina manyoya mazito yenye rangi ya kijivu hadi kahawia lakini rangi ya chini ni takriban nyeupe. Hula wanyama wa maji kama gegereka, wadudu, konokono wa maji, samaki na vyura.

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.

Makala hii kuhusu "Mmepulu" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili amepulu, katewe kutoka lugha ya Kiasoa, Kiluvale. Neno (au maneno) la jaribio ni mmepulu, katewe.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.