Fuko-dhahabu
Fuko-dhahabu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Fuko-dhahabu mkubwa (Chrysospalax trevelyani)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Nusufamilia 2, jenasi 9:
|
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mafuko-dhahabu au mafuko butu ni wanyama wa familia Chrysochloridae ambao wanachimba katika ardhi na kushinda takriban maisha yao yote chini ya uso wake. Wanyama wengine waitwao fuko ni wanafamilia wa Bathyergidae na Spalacidae (oda Rodentia), Talpidae (Soricomorpha) na Notoryctidae (Notoryctemorphia). Spishi zote za fuko-dhahabu zinatokea Afrika kusini kwa Sahara. Hula wadudu. Mafuko hawa huchimba mahandaki yao na miguu ya mbele iliyo na ukucha wa tatu ambao umevuvumulika. Vidole vya kwanza na vya nne vimebaki kama masalio na kile cha tano kimepotea. Miguu ya nyuma ina vidole vitano vyenye ngozi katikati. Macho yao hayafanyi kazi na yamefunika kwa ngozi. Masikio ni vipenyo vidogo tu.
Hali ya sasa
[hariri | hariri chanzo]Miongoni mwa spishi 21 za mafuko-dhahabu, angalau 11 zipo hatarini kwa kutoweka. Sababu za msingi ni uchimbaji wa mchanga, utendaji mbaya wa kilimo, ukuaji wa miji, na kuwindwa na mbwa na paka wa kufugwa.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Amblysomus corriae, Fuko-dhahabu wa Capetown (Fynbos golden mole)
- Amblysomus hottentotus, Fuko-dhahabu wa Natal (Hottentot golden mole)
- Amblysomus marleyi, Fuko-dhahabu wa Marley (Marley's golden mole)
- Amblysomus robustus, Fuko-dhahabu Imara (Robust golden mole)
- Amblysomus septentrionalis, Fuko-dhahabu Milimani (Highveld golden mole)
- Calcochloris leucorhinus, Fuko-dhahabu wa Kongo (Congo golden mole)
- Calcochloris obtusirostris, Fuko-dhahabu Njano (Yellow golden mole)
- Calcochloris tytonis, Fuko-dhahabu Somali (Somali golden mole)
- Carpitalpa arendsi, Fuko-dhahabu wa Arends (Arends's golden mole)
- Chlorotalpa duthieae, Fuko-dhahabu wa Duthie (Duthie's golden mole)
- Chlorotalpa sclateri, Fuko-dhahabu wa Sclater (Sclater's golden mole)
- Chrysochloris asiatica, Fuko-dhahabu Kusi (Cape golden mole)
- Chrysochloris stuhlmanni, Fuko-dhahabu wa Stuhlmann (Stuhlmann's golden mole)
- Chrysochloris visagiei, Fuko-dhahabu wa Visagie (Visagie's golden mole)
- Chrysospalax trevelyani, Fuko-dhahabu Mkubwa (Giant golden mole)
- Chrysospalax villosus, Fuko-dhahabu Manyoya-magumu (Rough-haired golden mole)
- Cryptochloris wintoni, Fuko-dhahabu wa De Winton (De Winton's golden mole)
- Cryptochloris zyli, Fuko-dhahabu wa Van Zyl (Van Zyl's golden mole)
- Eremitalpa granti, Fuko-dhahabu wa Grant (Grant's golden mole)
- Neamblysomus gunningi, Fuko-dhahabu wa Gunning (Gunning's golden mole)
- Neamblysomus julianae, Fuko-dhahabu wa Juliana (Juliana's olden mole)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Fuko-dhahabu wa Natal
-
Fuko-dhahabu wa Grant
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.