Mharagwe-pana
Jump to navigation
Jump to search
Mharagwe-pana (Vicia faba) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Miharagwe-pana shambani
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mharagwe-pana (Vicia faba) ni jina la mmea katika familia Fabaceae. Mbegu zake huitwa maharagwe mapana. Asili ya mmea huu ni Mashariki ya Kati lakini siku hizi hukuzwa mahali poti katika kanda za nusutropiki na wastani. Vipande vinavyolika ni mbegu (bichi na bivu), matumba machanga na majani.