Metodi wa Olimpo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Metodi wa Olimpo (alifariki mwaka 311 hivi) alikuwa askofu wa Olimpo (Lycia) na mfiadini kutoka Anatolia (leo nchini Uturuki).

Anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Taarifa za kwanza juu yake zimeandikwa na mtakatifu Jeromu[1]

Metodi aliandika sana na kwa ufasaha kuhusu masuala ya teolojia, akipinga uzushi wa wakati wake na hasa ule wa mafundisho kadhaa ya Origen.

Kwa bahati mbaya, vitabu vyake vimepotea kwa kiasi kikubwa. Kilichotufikia kizima kwa Kigiriki kinahusu ubikira (Symposion e peri hagneias).[2]

Kati ya matoleo ya maandishi yake kuna: Patrologia Graeca, XVIII; Jahn, S. Methodii opera et S. Methodius platonizans (Halle, 1865); Bonwetsch, Methodius von Olympus: I, Schriften (Leipzig, 1891).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. De viris illustribus, chapter 83
  2. In Patrologia Graeca, XVIII, 27-220.

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Metodi wa Olimpo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.