Mein Kampf

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Toleo la Kifaransa la "Mein Kampf"

Mein Kampf (Kijerumani: Mapambano au mapigano yangu) ni kitabu kilichoandikwa na Adolf Hitler kabla ya kushika utawala wa Ujerumani. Alieleza humo mawazo yake juu ya siasa, historia na dunia kwa jumla. Hitler alianzisha kitabu cha kwanza cha Mein Kampf gerezani alipofungwa baada ya jaribio la kupindua serikali mwaka 1923. Alipoondoka aliongeza kitabu cha pili. Tangu 1930 sehemu zote mbili zilichapishwa pamoja kama kitabu kimoja.

Katika kitabu chake Hitler alieleza kwa upana mawazo yake mbalimbali.

Yaliyomo ya kitabi kilikuwa

  1. alidai maungano ya Austria na Ujerumani
  2. alieleza kwa upana uadui wake dhidi ya Wayahudi akidai waliendesha ubepari lakini pia ukomunisti kwa shabaha ya kutawala dunia,
  3. alitangaza ujamaa au usoshalisti wa kitaifa badala ya ujamaa wa kimataifa akilenga kwa tabaka kubwa la wafanyakazi ya viwandani ;
  4. alieleza utawala wa ukomunisti katika Urusi ulipaswa kuondolewa kwa vita
  5. alidai ardhi katikia mashariki ya Ulaya kwa ajili ya Wajerumani ambao aliwaona walikosa nafasi waliostahili,
  6. alikashifu demokrasia kama muundo wa serikali na dola akidai ya kwamba utamaduni asilia wa Wajerumani ni mwenye kiongozi wa kitaifa mwenye mamlaka yote

Kitabu kilitangazwa kama "biblia" ya harakati ya Manazi. Baada ya Hitler kuwa kiongozi wa serikali na dikteta kilichapishwa na kugawiwa na vyombo vya serikali; bwana na bibi arusi wote walipewa nakala. Kwa jumla kilitolewa zaidi ya mara milioni kumi.

Baada ya mwisho wa utawala wake 1945 kitabu kilipigwa marufuku katika Ujerumani hadi leo. Mtu anaruhusiwa kuwa nacho lakini hakuna ruhsa kukichapisha upya.