Mawasilianoanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mawasilianoanga (tafsiri ya Kiing.-Kigiriki "telecommunication" kutoka Kigir. tele "mbali" Kiing. communication "kupeana habari, mawasilianio") ni kazi ya kupeana habari juu ya umbali tofauti na maongezi ya moja kwa moja kati ya watu walio karibu.

Zamani mawasiliano kwa umbali yalitekelezwa kwa msaada wa ngoma maalumu, alama za moto kutoka mlimani au alama za moshi zilizoonekana kwa mbali. Katika historia ya Ulaya au Asia kuna pia mifano ya semafori au heliografi (kioo cha kuakisisha nuru ya jua, kilichowekwa juu ya mnara au mlima). Inawezakana kutaja hapa pia nyaraka zilizosafirishwa kwa njia ya wakimbiaji au kwa watume waliopanda farasi.

Tangu karne ya 19 mitambo inayotumia umeme imechukua nafasi hii kama vile simu, televisheni, redio au intaneti.