Mataifa ya Kiturki
Mandhari
Mataifa ya Kiturki ni kundi la mataifa na makabila yanayotumia mojawapo ya lugha za Kiturki. Katika makala hii tunawaita "Waturki"[1]. Taifa kubwa katika kundi hilo ni Waturuki, raia wa nchi ya Uturuki.
Nchi nyingine ambako watu wengi ni kutoka mataifa ya Kiturki ni pamoja na Kazakhstan, Uzbekistan, Azerbaijan na Turkmenistan. [2]
Lakini wako pia katika Siberia (Urusi), katika milima ya Kaukazi, Iraki, Iran, Afghanistan, Kirgizia na China ya magharibi.
Wengi wao wanaweza kuwasiliana hata kama wanatoka nchi tofauti, kwa sababu lugha zao ni za karibu na kuna maneno mengi ya pamoja.
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mwanamume wa Altai aliyevaa suti ya kitaifa akiwa amepanda farasi.
-
Wasichana wa Azerbaijan katika mavazi ya jadi.
-
Wavulana wa Bashkortostan katika mavazi ya kitaifa.
-
Mcheza dansi wa Chuvashia akivaa mavazi ya kitamaduni.
-
Vijana na wazee wa Gagauzia .
-
Wazee wa Karachay katika karne ya 19.
-
Watu wa Khakasia na vyombo vya jadi.
-
Familia ya Kazakhstan ndani ya Yurti .
-
Mtu wa Dagestan katika vazi la taifa.
-
Wasichana wa Uturuki katika nguo zao za kitamaduni.
-
Mabinti wa Turkmen katika mavazi ya kitaifa.
-
Wanaume na wanawake huko Kyzyl, Tuva .
-
Watoto wa Uzbekistan huko Samarkand .
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Neno "Turki" ni jaribio na hadi sasa hakuna namna katika Kiswahili sanifu kutofautisha kati ya watu wa nchi ya Uturuki (tunawaita hapa Waturuki; Kiingereza Turks, people of Turkey) na watu wanaotumia mojawapo ya lugha tunazoita "za Kiturki" (Turkic languages, Turkic peoples). Kwa hiyo tunajaribu kutofautisha kati ya "Waturuki" wa Uturuki, na "Waturki" wanaotumia mojawapo ya lugha ambazo ni karibu kati yake.
- ↑ https://dergipark.org.tr/tr/download/article-file/785506