Masima bikira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Masima bikira (alifariki baada ya 484) ni kati ya wafiadini wa Kanisa Katoliki waliodhulumiwa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Genseriki aliyekuwa Mwario.

Akiwa mtumwa, aliwavutia katika Ukristo watumwa wenzake wanne, wote ndugu: Martiniani, Saturiani na wenzao.

Baada ya kutoroka, walijiunga na monasteri huko Thabraca, lakini walikamatwa na kuuzwa tena.

Wanaume walikopelekwa (Caprapicta) walivuta wengi katika Ukristo wa Kikatoliki[1], jambo lililosababisha chuki ya Waario hadi wakauawa.

Kumbe Masima aliachiliwa akawa abesi hadi kifo chake.

Habari zao zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 16 Oktoba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Stefano Antonio Morcelli, Africa christiana, Volume I, Brescia 1816, pp. 117–118
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.