Martiniani, Saturiani na wenzao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Martiniani, Saturiani na wenzao wawili walikuwa wote ndugu; ni kati ya wafiadini wa Kanisa Katoliki waliouawa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Genseriki aliyekuwa Mwario.

Wote waliongokea Ukristo kwa njia ya Masima bikira, mtumwa mwenzao.

Baada ya kutoroka, walijiunga na monasteri huko Thabraca, lakini walikamatwa na kuuzwa tena.

Huko walikopelekwa (Caprapicta) walivuta wengi katika Ukristo wa Kikatoliki[1], jambo lililosababisha chuki ya Waario hadi wakauawa pengine pamoja na wenzao 361, wakiwemo Saturnini, Nerei na Serea[2].

Habari zao zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 16 Oktoba[3][4][5][6].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.