Mashindano ya magari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mashindano ya magari ni aina ya michezo inayotumia motokaa. Ni kati ya michezo yenye watazamaji wengi duniani. Mashindano ya magari hufanywa kwenye viwanja maalumu au pia kwenye barabara za kawaida zilizOfungwa kwa muda kwa nyendo za kawaida.

Kuna mashindano ya motokaa za pekee zinazotegenezwa kwa mashindano tu, lakini pia mashindano mengine ya motokaa ya kawaida. Mashindano haya mara nyingi yanagharamiwa kwa kiasi kikubwa na makampuni yanayotumia nafasi hii kwa majaribio ya teknolojia za injini, matairi, breki au vipuli vingine.

Gari la mashindano ya 1894 Paris-Rouen

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mashindano ya kwanza ya magari yalifanywa mwaka 1894 huko Ufaransa kati ya miji ya Paris na Rouen kwa umbali wa kilomita 126. Yalitangazwa kama "mashindano ya magari bila farasi". Kati ya magari zaidi ya 100 ya mashindano yalikuwepo 39 zenye injini ya mvuke, 38 zenye injini ya petroli, 5 zenye injini ya umeme na 5 zilizoendeshwa kwa hewa iliyokandamizwa. Magari 15 tu yalifikia mwisho, mengine yalikwama njiani. Gari la kwanza likawa gari la mvuke la Albert Jules Comte de Dion lililofikia mbio wa 19 km/h kwa wastani.

Maendeleo ya teknolojia yalionyesha faida za injini ya petroli, hivyo injini nyingine zilipotea kwa muda mrefu katika mashindano ya magari.

Mashindano ya kwanza kwa umbali mkubwa ulitokea mwaka 1907 kati ya Beijing (China) na Paris kwa umbali wa takriban kilomita 15,000 na sehemu kubwa ya njia hii ilikuwa bila barabara. Motokaa 5 zilishiriki.

Magari ya fomula 1 kwenye Grand Prix huko Malaysia 2006

Aina za mashindano ya magari[hariri | hariri chanzo]

  • Mashindano ya fomula ambako magari yanayotimiza masharti fulani tu yanaruhusiwa. Aina inayojulikama zaidi ni "Fomula 1" . Mwaka 2014 masharti kwa washiriki yalikuwa kutumia injini ya silinda 6, mjao wa lita 1.6, mizunguko ya injini 15,000 kwa dakika na nguvu hadi 426 kW.
  • Mashindano ya Magari ya michezo (sports cars racing) ni pia magari yaliyotengenezwa hasa kwa ajili ya mashindano yao; hayana mbio kama fomula 1 lakini mashindano ni ya muda mrefu zaidi na kwa umbali mkubwa zaidi, kwa mfano mbio wa masaa 24 huko Le Mans ambako madereva 2 wanabadilishana.
Chevrolet Cruze touring
  • Mashindano ya Magari ya touring ni magari ya kawaida yaani yalitengenezwa viwandani kama motokaa ya barabarani ya kawaida lakini yanaandaliwa baadaye kwenye karakhana kwa ajili ya mashindano kwa kusahihisha injini, kubadilisha breki na kadhalika.
  • Mashindano ya rally hufanywa kwenye barabara za kawaida zilizofungwa kwa magari mengine ila washiriki au pasipo barabara. Kati ya rally mashuhuri ni Ralle Dakar ambayo kati ya 1978 hadi 2007 iliitwa Rallye Paris-Dakar kati ya Paris na Dakar (Senegal) na tangu 2009 hufanywa katika Amerika Kusini. Rally mashuhuri ya Afrika ya mashariki ni Safari Rally.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Mashindano ya magari kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.