Mary Sibande

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mary Sibande (11 Aprili, 1982) ni msanii wa Afrika Kusini anayeishi Johannesburg.

Sibande anafanya sanaa inayojumuisha uchongaji, picha pamoja na ubunifu. Anatumia sanaa yake kuelezea ukoloni, na zaidi sanaa yake katika Afrika na zaidi hutumia sanaa yake kuelezea ubaguzi wa rangi.[1] Sibande hutumia sanaa yake kukosa katika kukosoa matendo ya kisaniii ya wanawake hasa wanawake wa Afrika.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Sibande alizaliwa katika mji wa Barberton, Mpumalanga katika kipindi ambacho ubaguzi wa rangi ulikuwa umeshika nafasi ya juu, ambako alilelewa na bibi yake.[2] Baba yake alikuwa mwanajeshi katika jeshi la Afrika ya Kusini na Sibande hakuwahi kumfahamu baba yake katika kipindi cha utoto wake ,mama yake alikuwa akiendesha maisha yake kwa kufanya kazi za majumbani kwa sababu ya mama yake kuwa mfanyakazi wa majumbani, Sibande hueshimu sanaa na watu wanaofanya kazi za majumbani na moja kati ya sanaa zake maarufu ni ile inayompa heshima mwanamke iitwayo "Long Live the Dead Queen". [3] Sibande huelezea maisha yake ya utoto akisema "Nilikuwa na kila kitu ambacho nilikihitaji,nilisoma katika shule nzuri, nilikuwa na bahati ya kusoma katika shule ya aina hiyo, ambayo wazazi wengi walishindwa kuwapeleka watoto wao,hali hiyo ilinifanya mimi kuwa na muelekeo fulani wa maisha yangu"

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. name=":2">Bidouzo-Coudray, Joyce (7 January 2014). "Mary Sibande – poking at power relations in post-apartheid South Africa". The Guardian. Iliwekwa mnamo 28 April 2017.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  2. https://www.pressreader.com/south-africa/fairlady/20180401/282806421956976%7Ctitle=We sit down with internationally acclaimed artist Mary Sibande|first=Shireen |last=Fisher|date=1 April 2018}}
  3. "South African Artist Mary Sibande Has Solo Exhibit at Leroy Neiman Gallery | Columbia News". news.columbia.edu. Iliwekwa mnamo 2019-11-04. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mary Sibande kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.